Habari za Punde

Mama Mariam Mwinyi ashiriki Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge) Mhe. Ummy Nderiananga na Rais wa Jumuiya ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA) Dkt. Agnes Kalibata, alipowasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023 (AGRF) lililofanyika leo 6-9-2023, katika ukumbi huo
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Rais wa Jumuiya ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika ( AGRA) Dkt. Agnes Kalibata, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi mdogo wa jengo la Mikutano la Kimataifa la Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu, kabla ya kuaza kwa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023 (AGRF) uliyofanyika leo 6-9-2023 katika ukumbi huo.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023 (AGRF) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo 6-9-2023, na (kulia kwake) Waziri wa Maendeleo anayeshuhulikia Masuala ya Kimataifa Norway Mhe.Anne Beathe Tvinnereim.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia Mkutano wa Kimataifa Unaojadili Mfumo wa Chakula,unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo 6-9-2023, na (kulia kwake) Waziri wa Maendeleo anayeshuhulikia Masuala ya Kimataifa  wa Norway Mhe.Anne Beathe Tvinnereim na (kushoto kwake) Rais wa Jumuiya ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika ( AGRA) Dkt.Agnes Kalibata.
MKE wa Rais wa Zanzibar.Mama Mariam Mwinyi akizungumza na kutoa Mada juu ya nafasi ya Mwanamke katika Kilimo, wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023(AGRF) linalofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo 6-9-2023.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali na Wadau wa Kilimo, wanaohudhuria Mkutano wa Kimataifa unaojadili Mfumo wa Chakula kwa mwaka 2023 (AGRF) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo 6-9-2023 na (kushoto kwake) Rais wa Jumuiya ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika ( AGRA) Dkt.Agnes Kalibata na (kulia kwake) Waziri wa Maendeleo anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa wa Norway Mhe. Anne Beathe Tvinnereim.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.