Habari za Punde

Mhe.Spika Dkt.Tulia Amekutana na Kuzungumza na Naibu Waziri Mkuu Mhe.Dkt.Biteko

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 4 Septemba, 2023.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 4 Septemba, 2023.

 Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amemhakikishia Mhe.Biteko kuwa Bunge litampa ushirikiano wa kutosha ili kutimiza na  kufanikisha shughuli za Serikali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.