Beki wa Timu ya Jamhuri Abuu Ali akimpita mchezaji wa Timu ya Malindi Suleiman Hamad katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League 2023/2024" mchezo uliofanyika uwanja wac Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja.Timu ya Malindi imeshinda mchezo huo kwa bao 3-0.
MASARAHANGI wa timu ya soka ya Malindi wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao bao 3-0 dhidi ya Jamhuri katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliochezwa uwanja wa Mao Zedong A.
Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani kiasi ulichezwa majira ya saa 10 za jioni na kushuhudiwa na mashabiki wachache ambao waliridhika na burudani ya soka iliyokuwa ikioneshwa na wachezaji.
Katika mchezo huo miamba hiyo yote kwa pamoja ilikimaliza kipindi cha kwanza wakishindwa kufungana.
Hata hivyo kipindi cha pili kilianza na miamba hiyo ikaendelea kushambuliana na Malindi ikafanikiwa kupata mabao hayo ambayo yaliwafanya waondoke na pointi tatu.
Bao la kwanza la timu hiyo ambayo mechi yao ya kwaza wakitoka sare ya mabao 2-2 na timu ya Ngome lilifungwa na mchezaji wake Ramadhan Abdi Mponda dakika ya 66 ambae alifunga la pili dakika ya 85 na la tatu likafungwa na Seif Rajab mkenza dakika 86.
Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa kuchezwa michezo mitatu ambapo katika uwanja wa Mao Zedong A , JKU itacheza na Kundemba, Hard Rock na Kipanga watacheza uwanja wa Mao Zedong B na huko Finya Chipukizi itamkarobisha Ngome.

Mshambuliaji wa Timu ya Jamhuri Abdillahih Ramadhan akiwapita mabeki wa Timu ya Malindi (kushoto) Rajab Ali na (kulia) Omar Ame, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League 2023/2024" mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.Timu ya Malindi imeshinda mchezo huo kwa bao 3-0.
Mchezaji wa Timu ya Malindi Seif Rajab akimpita beki wa Timu ya Jamhuri Abdulraham Salum, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League 2023/2024" mchezo uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.Timu ya Malindi imeshinda mchezo huo kwa bao 3-0.
Mshambuliaji wa Timu ya Jamhuri Abdillahih Ramadhan akiwapita mabeki wa Timu ya Malindi Omar Ame, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League 2023/2024" mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.Timu ya Malindi imeshinda mchezo huo kwa bao 3-0.
No comments:
Post a Comment