Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Amefungua Mkutano wa Kimataifa wa Nishati

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,Dkt Doto Biteko  pamoja na viongozi wengine  alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua  Mkutano wa Tano wa Kimkataifa wa Nishati, Septemba 20, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Nishati. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wakati alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Nishati, Septemba 20, 2023. Kushoto kwake ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakishiriki kuimba wimbo wa Taifa  kabla ya kufungua Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Nishati kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es salaam
 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akizungumza katika  Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Nishati kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Nishati kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Nishati wakimsikiliza Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa alipofungua mkutano huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakimsikiliza Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha umeme wa Gesi ya SONGAS, Dkt.  Michael Mingodo (kulia) wakati alipotembelea banda la maonesho la kampuni hiyo baada kufungua Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Nishati kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko baada ya kufungua Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Nishati kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Septemba  20, 2023. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Felchesemi Mramba.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.