Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Dkt. Selemani Jafo akiwa katika kikao na Balozi wa Japan nchini
Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa wakati wa mazungumzo baina yao yaliyofanyika leo Septemba 14, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan hapa nchini, Mhe. Yasushi Misawa katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Septemba
14, 2023 Dkt. Jafo amemshukuru Balozi Misawa kwa juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali
ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo (JICA) kwa kuendelea
kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo maji, elimu, barabara, afya na
kuiomba Serikali hiyo kusaidia pia miradi ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira
iliyopo nchini.
Waziri Jafo amemueleza Balozi Misawa kuwa ajenda ya
mazingira ni moja ya kipaumbele muhimu vilivyopewa msukumo na Serikali ya Awamu
ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo Serikali kupitia
Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea na juhudi za kuhamasisha jamii kutumia
nishati mbadala ili kuhamasisha uhifadhi na utunzaji mazingira nchini.
“Tanzania tunazalisha takribani tani
Milioni moja za taka ngumu ambazo ni fursa ya uzalishaji wa nishati mbadala…tunatumia
asilimia 30 tu ya nishati hiyo…Tunahitaji nishati hii kwa ajili ya matumizi ya
kijamii na kiuchumi. Tunahitaji wawekezaji wengi zaidi kujitokeza kwa ajili ya
uwekezaji,” amesema Mhe. Dkt.Jafo.
Amesema kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi na rafiki
kwa wawekezaji na wadau wa nishati hiyo kuweza kujitokeza na kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati mbadala hususani katika maeneo ya vijijini ili kuongeza
upatikanaji wa nishati mbadala ya kupikia.
Waziri Jafo pia amemhakikishia Balozi Misawa
ushirikiano na utayari wa Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha utekelezaji
wa miradi ya nishati jadidifu
ikiwemo jotoardhi, tungamotaka, upepo na jua pamoja na matumizi bora ya Nishati mbadala ili kuleta manufaa
kwa wananchi na jamii kwa ujumla.
Akifafanua zaidi Waziri Jafo amesema Serikali
kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa sera, kanuni na miongozo mbalimbali ikiwemo
ikiwemo katazo Kwa taasisi zote za umma na binafsi kwa upande wa Tanzania Bara
zinazoandaa chakula na kulisha watu zaidi 300 kusitisha matumizi ya mkaa na
mkaa ifikapo mwaka Januari 2025.
Dkt. Jafo amesema kutokana na msisitizo huo,
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imendelea kuwahimiza wadau na
washirika wa maendeleo kujitokeza kuungana mkono juhudi hizo za serikali kwa
kuhakikisha zinaelekeza nguvu katika uwekezaji wa miradi ya nishati Rafiki kwa
mazingira.
Aidha kwa upande mwingine Dkt. Jafo ameiomba
Serikali ya Japan kutoa fursa ya ufadhili wa masomo kwa wataalamu wa mazingira
katika Ofisi ya Makamu wa Rais ili kuweza kujengewa uwezo wa kitaalamu na
kiufundi katika usimamizi wa miradi mbalimbali ya mazingira inayotekelezwa nchini.
Kwa upande wake, Balozi Misawa amemhakikishia Waziri Jafo kuwa Serikali
ya Japan itaendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo kwa kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza sekta ya Nishati hasa kwa
upande wa Nishati jadidifu.
Alisema, kuwa wawekezaji kutoka Japan wapo tayari kuja kuwekeza
nchini Tanzania katika sekta ya nishati jadidifu na kuhakiikisha kuwa
uwekezaji huo unaleta manufaa ya kijamii na kiuchumi baina ya Mataifa hayo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (kulia) akimkaribisha Balozi wa Japan Nchini
Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa
(katikati) mara baada ya kuwasili katika Ofisini kwake Mji wa Serikali Mtumba
Jijini Dodoma kwa ajili ya mazungumzo baina yao yaliyofanyika leo Septemba 14, 2023. Katikati ni Mshauri wa Uchumi
wa Ubalozi huo, Bw. Christopher Ntyangiri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Dkt. Selemani Jafo akiwa katika kikao na Balozi wa Japan nchini
Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa wakati wa mazungumzo baina yao yaliyofanyika leo Septemba 14, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akipokea kitabu utekelezaji wa miradi ya miradi ya maendeleo
inayotekelezwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) kutoka kwa
Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa mara baada ya mazungumzo
baina yao yaliyofanyika leo Alhamisi Septemba 14, 2023 katika Mji wa Serikali,
Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akimkabidhi nyaraka mbalimbali za taarifa kuhusu majukumu ya
Ofisi hiyo Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa mara baada ya
mazungumzo baina yao yaliyofanyika leo Septemba 14, 2023 katika Mji wa
Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa
katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan Mhe. Yasushi Misawa pamoja na
viongozi wengine mara baada ya mazungumzo baina yao yaliyofanyika leo Septemba
14, 2023 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa
katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan Mhe. Yasushi Misawa pamoja na
viongozi wengine mara baada ya mazungumzo baina yao yaliyofanyika leo Septemba
14, 2023 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na kuagana na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa pamoja na viongozi wengine mara baada ya mazungumzo baina yao yaliyofanyika leo Septemba 14, 2023 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
No comments:
Post a Comment