Habari za Punde

JK afurahishwa na wanawake kuupiga mwingi kwenye elimu UDSM

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mwenyekiti wa BAraza la Chuo hicho Balozi Mwanaidi Sinare Maajar baada ya kuhitimisha Duru la Pili la Mahafali ya 53 ya chuo hicho ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Alhamisi Oktoba 17, 2023

  Na Mwandishi Wetu


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema amefurahishwa sana kuona asilimia ya wahitimu wanawake chuoni hapo imefikia asilimia 54.7 na kuwashauri wanafunzi wanaume wafanye juhudi ili wasiachwe mbali sana na wenzao.

 

Akiongea kabla ya kuhitimisha Duru la Pili la Mahafali ya 53 ya chuo hicho, Dkt. Kikwete amesema kwamba kafurahishwa sana kuona wanawake siku hizi “wakiupiga mwingi” na kuwataka vijana wa kiume walichukulie jambo hilo kama changamoto kwa wao kufanya vizuri zaidi kwenye masomo.

 

Katika mahafali hayo yalifofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jumla ya wahitimu 2796 walihudhurishwa ikiwa ambapo 2700 walitunukiwa Shahada za Awali ikiwa ni wasichana 1488 na wavulana 1212.

 

Jumla ya Stashahada 78 zilitolewa kwa wanaume 45 na Wasichana 33, wakati wanaume 10 na wasichana wanane walitunukiwa Astashahada.

 

Makamu Mkuu wa Chuo Profesa William A.L. Anangisye aliwapongeza wahitimu wote huku akiwashauri watumie elimu waliyopata kuleta ushawishi chanya kwa watu wote wanaowazunguka na kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.

 

Profesa Anangisye aliwaasa wahitimu hao kwamba elimu waliyoipata ni mali ya umma na kwa mantiki hiyo ni lazima ilete faida kwa umma kwa Watanzania.

 

“Elimu haiwezi kuleta faida na kuwa chachu ya mabadiliko yaliyokusudiwa endapo kama haitatumika katika kutatua matatizo ya jamii”, alisema Profesa Ananngisye.

 

Makamu Mkuu huyo wa chuo aliendelea kushauri: “Endapo ajira serikalini au katika sekta binafsi zitachelewa kupatikana kuweni wepesi kuangalia sehemu nyingine ambapo maarifa na ujuzi wenu unaweza kutumika kwa ufanisi Zaidi…

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.