1. Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimkabidhi
nakala ya mwongozo wa Ukaguzi wa Mazingira kwa Miradi ya Ujenzi wa Majengo
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),
Dkt. Samuel Gwamaka muda mfupi mara baada ya uzinduzi wa mwongozo huo wakati wa
hafla iliyofanyika leo Jumatano (Oktoba 18, 2023) katika
Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya NEMC, Prof. Eng.
Esnati O. Chaggu
Na Mwandishi Wetu. OMR, DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuongeza wigo wa kuandaa miongozo ya tathimini ya
athari za mazingira (TAM) kupitia sekta za viwanda, nishati, kilimo na maji ili
kuharakisha zoezi la mapitio ya miradi ya tathimini za athari kwa mazingira.
Akizungumza leo Jumatano (Oktoba 18, 2023) Jijini
Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa ukaguzi
wa mazingira kwa miradi ya ujenzi wa majengo ulioandaliwa na NEMC kwa
kushirikiana na Kituo cha Sayansi na Mazingira cha Nchini India (CSE), Dkt.
Jafo amesema uhifadhi na usimamizi wa mazingira ni mojawapo ya maeneo ya
vipaumbele vilivyopo katika malengo makuu ya Serikali.
Dkt. Jafo amesema mwongozo ambao umezingatia mahitaji halisi ya nchi
ikiwemo ukuaji wa miji na majiji, limeipa NEMC mamlaka ya kuhakikisha hali ya mazingira inaboreshwa
nchini kwa kusaidia uboreshaji wa afya ya jamii ikiwa ni pamoja na mazingira
vinalindwa na kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini.
‘’Kipengele
Na. 17 cha Makubaliano ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo Endelevu
unazitaka nchi wanachama kuhusisha tathmini za athari za mazingira katika miradi
ambayo inasababisha madhara kimazingira…. katika kutekeleza kipengele hicho zilianzisha
taasisi, na kutengeneza Sera na Sheria ikiwa ni pamoja na Kanuni kama ilivyo
kwenye Kanuni ya Athari ya Mazingira za Mwaka 2005 na zile za Mwaka 2018’’
amesema Dkt. Jafo.
Kwa mujibu wa Waziri Jafo
amesema Tathmini za Athari kwa Mazingira
(TAM) hufanyika ili kuweka mifumo bora ya kulinda mazingira ikiwa ni pamoja na
kupunguza kiwango cha taka zinazozalishwa, kutoa kipaumbele katika masuala ya
jamii, kuainisha athari zilizopo na madhara yanayoweza jitokeza kutokana na
miradi inayoanzishwa.
Waziri Jafo amesema NEMC inapokea zaidi ya miradi 2000 kwa mwaka kwa ajili ya
mapitio na kuongeza kuwa idadi hiyo ya miradi ni kubwa na itaweza kupitiwa kwa
ufanisi iwapo kutakuwa na miongozo ya kila sekta kama inavyoelekezwa katika Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.
Dkt. Jafo ameishukuru
Serikali ya India kupitia kituo hicho kwa kushirikiana na NEMC katika kuandaa
mwongozo huo kwani ushirikiano huo ni ishara ya ya matokeo ya ushIrikiano wa
taasisi hizo katika kupatia ufumbuzi wa changamoto za kimazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Kituo cha Sayansi na Mazingira cha Nchini India (CSE), Nivit Yadav amesema
Tanzania ni nchi ya tatu Bara la Afrika yenye kasi kubwa ya idadi ya watu na
nchi ya pili kwa Mataifa ya Afrika Mashariki kuwa na kasi ya ukuaji wa sekta ya
ujenzi, hivyo suala la tathmini ya miradi ya ujenzi ni jambo muhimu linalopaswa
kupewa kipaumbele katika uhifadhi na usimamizi wa mazingira.
Amesema Sheria ya Uhifadhi
na Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 imeanisha vipaumbele mbalimbali vya
utekelezaji wa Sheria hiyo ikiwemo kanuni na miongozo ya utekelezaji ikiwemo
ushirikiano baina ya Serikali w ikiwemo NEMC na CSE.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samwel Gwamaka
amesema kwa muda mrefu kumekuwepo na changamoto ya usimamizi wa tathmini ya
athari kwa mazingira kupitia maandiko ya miradi mbalimbali yanayowasilishwa kwa
ajili ya utoaji wa vibali vya mazingira.
“Awali wataalamu wetu
hawakuwa na mwongozo wa maandiko ya tathmini ya miradi ya athari za mazingira
ambayo inakidhi matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na kanuni
zake….Baada ya uzinduzi huu sasa wataalamu elekezi wa mazingira na wadau
watakuwa na mwongozo wa uaandaji wa maandiko kwa kuzingatia viwango na ubora
unaohitajika” amesema Dkt. Gwamaka.
. Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (wa tatu
kutoka kulia) pamoja na Watendaji na Viongozi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Kituo cha Kituo cha Sayansi na Mazingira cha Nchini
India (CSE) wakionesha nakala ya mwongozo wa ukaguzi wa Mazingira kwa Miradi ya
Ujenzi wa Majengo muda mfupi baada ya uzinduzi wa mwongozo huo. Hafla hiyo
ilifanyika leo Jumatano (Oktoba 18, 2023) katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini
Dodoma
. Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Mkurugenzi wa
Mradi wa Kituo Kituo cha Sayansi na Mazingira cha Nchini India (CSE) Bw. Nivit
Yadav (anayezungumza) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa Ukaguzi wa
Mazingira kwa Miradi ya Ujenzi wa Majengo baina ya NEMC na Kituo cha Sayansi na
Mazingira, Nchini India (CSE). Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatano (Oktoba 18,
2023) katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
1. Mkurugenzi wa
Tafiti za Mazingira wa Baraza la Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC), Dkt. Menan Jangu akizungumza jambo wakati wa wa
hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa Ukaguzi wa Mazingira kwa Miradi ya Ujenzi wa
Majengo baina ya NEMC na Kituo cha Sayansi na Mazingira, Nchini India (CSE).
Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatano (Oktoba 18, 2023) katika Mji wa Serikali,
Mtumba Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Mradi wa Kituo Kituo cha
Sayansi na Mazingira, Nchini India (CSE) Bw. Nivit Yadav.
1. Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo
(kushoto) akibadilishana mawazo na Watendaji Waandamizi wa Kituo cha Kituo cha
Sayansi na Mazingira cha Nchini India (CSE) kutoka kulia Shobhit Srivastava,
Naibu Meneja Mkurugenzi na Bw. Nivit Yadav, Mkurugenzi wa Mradi muda mfupi baada ya uzinduzi wa mwongozo wa wa ukaguzi wa Mazingira kwa Miradi ya Ujenzi
wa Majengo. Hafla hiyo ilifanyika katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma
leo Jumatano (Oktoba 18, 2023).
1. Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo akiwa katika
picha ya pamoja na na Watendaji na Viongozi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Kituo cha Kituo cha Sayansi na Mazingira cha
Nchini India (CSE) muda mfupi baada ya uzinduzi wa mwongozo wakionesha nakala
ya mwongozo wa ukaguzi wa Mazingira kwa Miradi ya Ujenzi
wa Majengo. Hafla hiyo ilifanyika katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma
leo Jumatano (Oktoba 18, 2023).
No comments:
Post a Comment