Habari za Punde

Rais DK Hussein Mwinyi afungua mkutano wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na fedha


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea katika ukumbi wa mkutano katika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na Masuala ya Fedha na Jinsia kutoka nchi 22 wanachama wa Jukwaa la Usawa wa Kijinsia (UN Women) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-Afritac East) na (kulia kwa Rais) Waziri wa Fedha na Mipango Tanzania Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila.(Picha na Ikulu)
WASHIRIKI wa Mkutano wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na Masuala ya Fedha na Jinsia kutoka Nchi 22 Wanachama wa Jukwaa la Usawa wa Kijinsia (UN Women) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-Afritac East) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuufungua mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam leo 15-11-2023, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua Mkutano wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na Masuala ya Fedha na Jinsia kutoka Nchi 22 Wanachama wa Jukwaa la Usawa wa Kijinsia (UN Women) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-Afritac East) unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam leo 15-11-2023, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Tanzania imepitisha na kutekeleza mageuzi kadhaa ya kisera yakiwemo marekebisho ya hivi karibuni ya sera ya maendeleo ya jinsia ya Tanzania ambayo yameweka mfumo wa kuimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake katika masuala ya elimu, afya, ajira na upatikanaji wa ardhi.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akifungua mkutano wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na fedha pamoja na jinsia kutoka nchi 22 wanachama kwa kushirikiana na jukwaa la usawa wa kijinsia(UN WOMEN) na shirika la fedha la kimataifa (IMF Afritac East) ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana, Dar es Salaam.

Naye Waziri wa fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ni nguzo ya mafanikio kwa Wanawake nchini kutokana na uongozi wake, pia Serikali imeendelea kupigania usawa wa kijinsia na kuwawezesha Wanawake nchini.

Nchi zinazoshiriki mkutano huo ni pamoja na wenyeji Tanzania, Burundi, Burkina Faso, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Eritrea, Ethiopia, Guinea, Ivory Coast, Nigeria, Senegal, Kenya,  Liberia, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Somalia, Afrika Kusini, Rwanda, Sudan ya Kusini, Zambia, Zimbabwe na Uganda.

Mkutano huo wa siku tatu utajadili mambo mbali mbali yanayohusu ufadhili wa usawa wa kijinsia ambapo mashirika mbalimbali ya kimataifa wanashiriki mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.