Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi azindua boti mpya ya "ZANZIBAR III inayomilikiwa na Kampuni ya Zan Fast Ferries bandari ya Mkoani


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati alipowasili katika Bandari ya Mkoani kuzindua Boti mpya ya "ZANZIBAR III ya Kampuni ya Zan Fast Ferries Leo akiwa katika mwendelezo wa ziara ya Mikoa ya Pemba katika Shamra Shamra ya kutimiza Miaka mitatu ya Uongozi wake.[Picha na Ikulu] 01/11/2023. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akikata utepe kuzindua Boti mpya ya "ZANZIBAR III inayomilikiwa na Kampuni ya Zan Fast Ferries,hafla iliyofanyika leo katika Bandari ya Mkoani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba akiwa katika mwendelezo wa ziara zake katika Shamra Shamra ya kutimiza Miaka mitatu ya Uongozi wake.[Picha na Ikulu] 01/11/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatana na  Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakati alipotembelea sehemu mbali mbali mara baada ya kuizindua Boti mpya ya "ZANZIBAR III inayomilikiwa na Kampuni ya Zan Fast Ferries,hafla iliyofanyika leo katika Bandari ya Mkoani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba akiwa katika mwendelezo wa ziara zake katika Shamra Shamra ya kutimiza Miaka mitatu ya Uongozi wake.[Picha na Ikulu] 01/11/2023. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  na  Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiwa katika chumba cha Kepteni wa Boti mpya ya "ZANZIBAR IIalipotembelea sehemu mbali mbali mara baada ya kuizindua  rasmi leo boti hiyo inayomilikiwa na Kampuni ya Zan Fast Ferries,itafanya safari zake Pemba-Zanzibar-dar es Salam nna Tanga,hafla ya uzinduzi ilmefanyike leo  Bandari ya Mkoani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, akiwa katika mwendelezo wa ziara zake katika Shamra Shamra ya kutimiza Miaka mitatu ya Uongozi wake.[Picha na Ikulu] 01/11/2023.  No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.