Na.Maulid Yussuf
Mkurugenzi Idara ya Mipango Sera na Utafiti BDaima Mohamed Mkalimoto amesema kuna umuhimu wa uratibu wa usimamizi wa pamoja wa uanzishwaji wa wadau wanaohusina na jukwaa la watoto ili kuweza kutoa huduma bora za watoto katika hali tofauti.
Amesema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau kutoka katika sekta ya umma, sekta binafsi na Washirika wa Maendeleo, kuhusu uanzishwaji wa jukwaa la wadau wanaoshughulikia maendeleo ya watoto Zanzibar. katika ukumbi wa UN Agency katika jengo la uwekezaji ZSTC Kinazini Mjini Unguja.
Amesema hatua hiyo itasaidia kuwaweka pamoja katika uratibu wa utekelezaji wa shughuli zinazogusa Maendeleo ya watoto nchini.
Amewaomba wadau hao kutoa maoni yao katika mkutano huo ili kuhakikisha yanaingizwa katika mapendekezo ya kuanzishwa kwa jukwaa hilo, ili yaweze kufanyiwa kazi.
Akiwasilisha mapendekezo ya kuanzishwa jukwaa la wadau wanaoshughulikia Maendeleo ya watoto Zanzibar, Mshauri elekezi kutoka Shirika la UNICEF na Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Hurua Tanzania Dr Ladislaus Batinoluho ameipongeza Zanzibar kwa hatua nzuri iliyofikia kutokana na kazi kubwa wanayoifanya katika kuwahifadhi watoto.
Amesema pamoja na mafanikio hiyo, bado watoto wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo utumikishwaji kwa watoto, kudhalilishwa, na kubakwa.
Nao washiriki wa mkutano huo, wameshauri kuanza taratibu za kuanzishwa jukwaa la wadau kwa kuwashirikisha wadau na taasisi zote zinazowahusu watoto wakiwemo Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya pamoja ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwa jukwaa hilo.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO.
No comments:
Post a Comment