Habari za Punde

Maonesho ya Kazi Zinazofanywa na Taasisi za Serikali na Binafsi

Waziri wa Nchi (OR) Kazi,uchumi na uwekezaji akitoa taarifa kuhusina na maonesho ya  kazi zinazofanywa na taasisi za umma na binafsi kupitia magari.

Picha na Fauzia Mussa - Maelezo Zanzibar. 

Na Imani Mtumwa, Maelezo Zanzibar

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amewataka  wananchi kujitokeza kwa wingi katika barabara  kuyapokea na kuyasherehekea maonesho ya kazi zinazofanywa na Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na maonesho hayo huko Ofisini kwake Mwanakwerekwe amesema kwa mara ya kwanza Wizara hiyo imeandaa maonesho hayo yanayotarajiwa kufanyika januari 4 mwaka huu ili kutatoa fursa kwa taasisi hizo kutangaza kazi zao pamoja na wananchi  kuona kazi zinazofanywa na taasisi hizo.

Mhe. Mudrik ameeleza kuwa maonesho hayo yanatarajiwa kupokelewa na Makamo wa Pili wa Rais Mstaafu wa awamu ya saba Mhe. Balozi Seif Ali Iddi katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge ambapo magari hayo yatatoa huduma mbalimbali kwa wananchi viwanjani hapo.

Alifahamisha kuwa magari hayo yatapita barabarani kuanzia Amani kupitia  Mikunguni kwa Pweza, Saateni, Pinda Mgongo, Malindi, Darajani, Kisiwandui, Michenzani, Kisonge, Kariakoo na kurudia Michenzani na baadae kupitia Madema na kumalizia katika viwanja vya Maisara kuanzia saa 7:30 za mchana hadi saa 12:00 za jioni.  

Maonesho hayo yameandaliwa na Wizara ya nchi (OR), Kazi, Uchumi na Uwekezaji kwa kushirikiana na Mkoa wa Mjini Magharibi kuelekea maadhimsho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufikia kilele chake Januari 12.

 


MAELEZO YA PICHA


Waziri wa Nchi (OR) Kazi,uchumi na uwekezaji akitoa taarifa kuhusina na maonesho ya  kazi zinazofanywa na taasisi za umma na binafsi kupitia magari.

PICHA NA FAUZIA MUSSA - MAELEZO 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.