Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza lav Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Ajumuika na Wananchi katika Iftari Ukumbi wa GoldenTulip Zanzibar

RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na  Alhajj Ahmad  Al falasi , alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki  Wilaya ya Magharibi “B” Unguja  kuhudhuria Futari iliyoandaliwa na Alhajj Alfalasi katika ukumbi wa hote hiyo 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Zanzibar katika futari maalum iliyoandaliwa na Alhajj Ahmad Al falasi (kulia kwa Rais) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar jana 20-3-2024 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutowa shukrani kwa waandalizi wa futari maalumu iliyoandaliwa na Alhajj Ahmad Al falasi kwa Wananchi wa Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar jana 20-3-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi na Viongozi katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zazibar, Sheikh Saleh Omar Kabi baada ya kumalizika kwa futari maalum iliyoandaliwa na Alhajj Ahmad Al falasi (kulia kwa Rais) na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh, iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar jana 20-3-2024 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.