Habari za Punde

Mhe Waziri Jafo Awasili Kativi Kuanza Safari ya Kuelekea Wili ya Mazingira

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasili mjini Mpanda mkoani Katavi kwa ajili ya ziara ya kikazi leo tarehe 28 Mei, 2024.

Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa shughuli mbalimbali zinazotekelezwa chini ya Mradi wa Urejeshaji wa Uoto wa Asili unaotekelezwa katika mikao mbalimbali nchini.

Uzinduzi huo ni sehemu ya shamrashamra za kuadhimisha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni tarehe 5 Mei, 2024.

Shughuli zitakazozinduliwa ni pamoja na josho la mifugo, banio na birika la kunyweshea mifugo maji. Pia, kutakuwa na shughuli za kugawa hati miliki za ardhi za kimila 4450 pamoja na hati ya msitu.

Mikoa ambayo mradi huo unatekelezwa Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa na Katavi katika wilaya saba.

Waziri Jafo aliyeambatana na viongozi na watalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais amepokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Bw. Albert Msovela.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.