Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Amejumuika na Wananchi Katika Maziko ya Muasisi wa UWT Marehemu Asha Simba Makwega

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi na Viongozi  mbalimbali katika Sala ya Maiti ya Marehemu Asha Simba Makwega Muasisi wa UWT pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Sala hiyo iliyoongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, iliyofanyika katika Msikiti wa Maisara Wilaya ya Mjini Unguja na kuzikwa Kijijini kwao Pete Mkoa wa Kusini Unguja leo 8-5-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi na Viongozi  mbalimbali katika kuitikia dua ikisomwa na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Mahmoud Mussa Wadi, ya kumuombea Marehemu Asha Simba Makwega Muasisi wa UWT pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,baada ya kumlizika kwa Sala hiyo iliyofanyika,katika Msikiti wa Maisara Wilaya ya Mjini Unguja na kuzikwa Kijijini kwao Pete Mkoa wa Kusini Unguja leo 8-5-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka udongo katika kaburi likiwa na mwili wa marehemu Asha Simba Makwega, Muasisi wa UWT pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, wakati wa maziko yake yaliyofanyika kijijini kwao Pete Mkoa wa Kusini Unguja leo 8-5-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kutowa mkono wa pole kwa Wanafamilia ya Marehemu Asha Simba Makwega, baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Pete Mkoa wa Kusini Unguja leo 8-5-2024
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.