RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imefanya mambo mengi na kuboresha sekta mbalimbali za
maendeleo ikiwemo kuleta mageuzi makubwa kwenye miundombinu ya Afya, Elimu na
Maji safi.
Amesema ujenzi wa skuli na hospitali za ghorofa kwa
Wilaya zote za Unguja na Pemba na majimbo yote ya Zanzibar kuenea skuli za
kisasa, kuimarishwa kwa miundombinu ya maji safi kwa ujenzi wa matangi ya maji
na kuenezwa visima ili kuwaondoshea wananchi adha ya huduma za jamii sambamba
na ujenzi wa barabara zenye kiwango cha lami.
Alhajj Dk. Mwinyi aliyasema hayo
kwenye Ibada ya Sala ya Ijumaa na dua maalumu aliyoandaliwa na wananchi wa
wazee wa Vijiji vya Ukongoroni na Charawe ikiwa ni sehemu ya shukurani yao baada
ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Ukongoroni hadi Charawe pamoja na
kuipongeza Serikali kwa hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa kwenye kukuza
huduma za jamii nchini.
Akizungumzia ujenzi wa Skuli ya Mkoa ya Binguni kubwa
ya Rufaa ya Binguni Mkoa wa Kusini Unguja, tayari fedha za matengenezo
zimepatikana.
Aidha, Alhajj Dk. Mwinyi
amewaahidi wananchi wa Mkoa huo Ujenzi wa barabara ya Tunguuu hadi Makunduchi kwa mwendelezo wa
barabara hiyo iliyoishia Tunguu.
Alisema, Serikali imeazimia kujenga njia mbili kulia
na kushoto na taa za barabarani chini ya kampuni ya Brazil, aidha Alhajj Dk. Mwinyi ameridhia ombi
la wananchi wa Chwaka kujengewa daraja kwenye barabara ya Chwaka.
Pia, Alhajj Dk. Mwinyi
aliwashukuru wananchi kwa Mkoa
wa kusini Unguja kwa shukurani zao na dua ya kuombea maendeleo makubwa kwa Serikali
yao.
Sambamba na hilo pia aliwaasa waumini na wananchi wa
Mkoa huo kuenedela kuliombea taifa kwa mambo makubwa mawili ikiwemo kuendelea
watu kuishi kwa amani na mshikamano pamoja na kuendelea kuwaombea dua viongozi kwa kuyatekeleza yote
waliyowaahidi.
Akizungumza kwenye ibada ya Sala ya Ujumaa na dua ya
kuwaombea viongozi wa Serikali, Khatibu wa Ibada hiyo, aliwashajihisha wananchi
na waumini wa dini ya kiislamu, kuwaombea dua njema viongozi wao kwa Mwenyezi
Mungu awawafikishe kwenye mambo ya kheir.
Alisema,
Waislamu wamepewa miongozo ya dini kwenye utaratibu wao wa uongozi,
ambao ni wajibu wa wanaoongozwa kuishi kwa wema na viongozi wao kwa kuwatii kwa
mambo yasiyomuasi Mwenyezi Mungu, kuwaheshimu, kuwasifia kwa mazuri yao, kwenye
utekelezaji wa majukumu yao.
Alisema, ubora wa viongozi uko kwa wanaongozwa kuwajali
na kuwapenda viongozi wao.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment