Habari za Punde

SHIRIKA LA BIMA CHINA LAWEKA NIA UGHARAMIAJI RELI YA KISASA

Kikao kati ya Ujumbe wa Tanzania uliiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Ujumbe kutoka Shirika la Bima la China (China Export and Credit Insurance Corporation (SINOSURE), uliofanyika jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano hususani kwenye eneo la ugharamiaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambapo shirika hilo linaendelea na taratibu za upatikanaji fedha za kugharamia ujenzi wa Kipande cha Tano na Sita cha Reli hiyo kutoka Isaka hadi Mwanza chenye urefu wa Kilomita 341 na Tabora hadi Kigoma chenye urefu wa zaidi va Kilomita 411.

Ujumbe kutoka Shirika la Bima la China (China Export and Credit Insurance Corporation (SINOSURE) wakimsikiliza kwa umakini Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao cha ujumbe huo na Ujumbe kutoka Tanzania, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano hususani kwenye eneo la ugharamiaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambapo shirika hilo linaendelea na taratibu za upatikanaji fedha za kugharamia ujenzi wa Kipande cha Tano na Sita cha Reli hiyo kutoka Isaka hadi Mwanza chenye urefu wa Kilomita 341 na Tabora hadi Kigoma chenye urefu wa zaidi va Kilomita 411.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tano kulia) na Meneja Msaidizi wa Shirika la Bima la China (China Export and Credit Insurance Corporation (SINOSURE), Bi. BI Xiaonan, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Serikali ya Tanzania na Taasisi hiyo, mara baada ya kumalizika kwa kikao chao jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano hususani kwenye eneo la ugharamiaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambapo shirika hilo linaendelea na taratibu za upatikanaji fedha za kugharamia ujenzi wa Kipande cha Tano na Sita cha Reli hiyo kutoka Isaka hadi Mwanza chenye urefu wa Kilomita 341 na Tabora hadi Kigoma chenye urefu wa zaidi va Kilomita 411.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kulia), akiagana na Meneja Msaidizi wa Shirika la Bima la China (China Export and Credit Insurance Corporation (SINOSURE), Bi. BI Xiaonan, mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo, jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano hususani kwenye eneo la ugharamiaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambapo shirika hilo linaendelea na taratibu za upatikanaji fedha za kugharamia ujenzi wa Kipande cha Tano na Sita cha Reli hiyo kutoka Isaka hadi Mwanza chenye urefu wa Kilomita 341 na Tabora hadi Kigoma chenye urefu wa zaidi va Kilomita 411.

Na. Peter Haule, WF, Dodoma

Shirika la Bima la China - (China Export and Credit Insurance Corporation (SINOSURE) linaendelea na taratibu za upatikanaji fedha za kugharamia ujenzi wa Kipande cha Tano cha Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Isaka hadi Mwanza chenye urefu wa Kilomita 341 na kuonesha nia ya kusaidia upatikanaji fedha za ujenzi wa kipande cha sita cha ujenzi wa Reli hiyo kutoka Tabora hadi Kigoma chenye urefu wa zaidi ya Kilomita 411.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Shirika la Bima la China (SINOSURE), ukiongizwa na Meneja Msaidizi wa Shirika hilo, Bi.  Bi Xiaonan.

Dkt. Nchemba amelishukuru Shirika la SINOSURE kwa kuendelea na taratibu za upatikanaji fedha za ukamilishaji wa mradi huo kwa kuwa vipande hivyo ni muhimu katika ukamilishaji wa mradi huo.

“Tumekuwa na kikao kizuri katika kujadiliana ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na China hususan  kwenye eneo la ugharamiaji wa miradi ya kimkakati ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa Kipande cha Tano kutoka Isaka hadi Mwanza ambapo SINOSURE ilikubali kushiriki katika upatikanaji wa fedha wa kukamilisha ujenzi huo na kipande cha Tabora hadi Kigoma”, alisema Dkt. Nchemba.

Alisema Wizara ya Fedha kwa niaba ya Serikali inawahakikishia SINOSURE na Serikali ya China kwamba itaendeleza  ushirikiano na kuimarisha Maendeleo ya Uchumi kwa manufaa ya wananchi wa pande hizo mbili.

Dkt. Nchemba alisema kuwa Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha itaendelea kushirikiana na Timu kutoka Shirika hilo ili kuhakikisha vipande hivyo muhimu vinakamilika. 

Alisema kuwa Reli ni moja ya miradi ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeuweka kwenye miradi ya kielelezo na kipaumbele.

Aidha, ameshukuru ujio wa Meneja huyo Msaidizi wa SINOSURE pamoja na utayari wa Shirika hilo kushirikiana na Serikali katika ugharamiaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa Shirika la Bima la China (SINOSURE), Bi.  Bi Xiaonan, amesema Shirika lake lipo tayari kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha miradi ya kimkakati inatekelezwa kwa ufanisi.

Aidha alieleza kuwa Shirika lake linaendelea kufanyia kazi  namna ya upatikanaji fedha za kugharamia vipande hivyo na wapo katika hatua nzuri ya utekelezaji na taarifa zitatolewa kuhusu hatua iliyofikiwa.

Wizara ya Fedha katika kuhakikisha inapata fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, imeendelea na jitihada za kuwashirikisha wadau wake ili kugharamia utekelezaji wake ili malengo yake ya kuimarisha usafiri na usafirishaji wa mizigo na abiria uweze kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa na mwananchi mmoja mmoja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.