Habari za Punde

‘Waliotafuna ’ Milioni 39.5 Kibaoni Kuchukuliwa Hatua

 

Mkuu wa wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Alhaji Majid Mwanga akizungumza wakati wa uwasilishaji taarifa ya ukaguzi wa mapato na matumizi kutokana na migogoro ya ardhi katika kijiji cha Kibaoni halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe katika wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bi. Shamim Daud akisoma taarifa ya uchunguzi wa Mapato na Matumizi kutokana na migogoro ya ardhi katika kijiji cha Kibaoni.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akizungumza katika mkutano wa hadhara kupokea taarifa ya uchunguzi wa Mapato na Matumizi kutokana na migogoro ya ardhi katika kijiji cha Kibaoni hamashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.
(PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

Na Munir Shemweta, MLELE.

Mkuu wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi Alhaji Majid Mwanga 

amesema wahusika wote wa ubadhilifu wa fedha shilingi 

39,501, 665 katika kijiji cha Kibaoni halmashauri ya Mpimbwe 

wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi watachukuliwa hatua kwa 

mujibu wa sheria.


Alhaji Mwanga ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara 

na wananchi wa kijiji cha Kibaoni wakati wa uwasilishaji 

taarifa ya uchunguzi wa mapato na matumizi iliyotokana na 

migogoro ya ardhi katika kijiji cha Kibaoni iliyosomwa na 

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mpimbwe Bi. 

Shamim Daud.


‘’Hatutamfumbia macho mtu hata tone moja, baadhi ya 

viongozi wa kijiji na wao wamehusika kwenye upotevu wa 

milioni 39, 501, 665 wote hao walihusika lakini na watu 

ambao ni nje ya serikali ya kijiji walihusika kama ilivyosemwa 

mmoja wa watumishi yuko kampuni hiyo’’. Alisema Alhaji 

Majid Mwanga.


Akiwasilisha taarifa ya uchunguzi wa mapato na matumizi 

iliyotokana na migogoro ya ardhi kwenye kijiji cha Kibaoni, 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya 

Mlele Bi. Shamim Daud amesema, maeneo yaliyohusika 

katika ubadhilifu ni pamoja na eneo la shule mpya ya Kibaoni 

ambapo wakati wa kupatikana kwake ilipunguzwa ekari 3 na 

kuwa 15 badala ya ekari 18.


Eneo lingine kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo Mtendaji wa 

halmashauri ya Mpimbwe Bi.Shamim ni la Viwanda Vidogo la 

SIDO ambapo fedha kiasi cha shilingi milioni 8.8 kwa ajili ya 

mauzo ya viwanja 48 hazikupelekwa benki na hakuna 

matumizi yoyote yaliyoonekana ya shughuli za serikali.


Aidha, makusanyo ya mapato ya shilingi 21,240,000 kutoka 

vyanzo vya mapato mbalimbali ya kijiji cha Kibaoni  

yanayojumuisha michango ya jamii, kukodisha mashamba, 

tozo na faini mbalimbali kiasi kilichopelekwa benki kati ya 

jumla ya milioni 21,240,000 ni shilingi milioni 2 tu huku 

kisichopelekwa benki ni 1,9210,000.


‘’Kumetokea pia ubadhilifu wa fedha za kijiji kutoka katika 

akaunti yake ya jumla ya milioni 2.80 zilizotolewa katika 

kaunti kwa ajili ya kurejesha kwa watu 39 wakati hakuna 

fedha yoyote iliyoingizwa kutokana na tukio hilo’’. Alisema Bi. 

Shamim.

Kuhusu malipo ya fidia kwa serikali ya kibaoni kutokana na 

maeneo ya wananchi kuchukuliwa kwa ajili ya kuchimba 

vifusi na kuchukua udongo kwa ajili ya ujenzi wa barabra ya 

kibaoni- Sitalike, amesema pamoja na kijiji cha Kibaoni 

kupokea shilingi milioni 21 kutoka kampuni ya RSG Ltd na 

wananchi wawili nao kufidiwa lakini pesa zote hazikupelekwa 

benki. Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi baadhi ya viongozi 

wa kata, watendaji wa vijiji na watumishi wa kampuni ya RSG 

walishiriki kugawana fredha za fidia.


Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kibaoni wametaka hatua za 

kisheria zichukuliwe kwa wote waliohusika kwenye ubadhilifu 

wa fedha ikiwemo kurejesha fedha walizochukua.


‘’Hizi pesa zote zirudi ili kupunguza msongamano wa mizigo 

iwe kuuzwa nyumba, iwe kiwanja au kufanya nini pesa zote ili 

anayekuja leo kibaoni ajue anapodokoa hata hata mia tano ya 

kula ya wizi ajue hii ni pesa inayoweza kuniunguza’’ alisema 

Mathelius Matabula.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na 

Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, 

Geophrey Pinda ametaka sheria ifuate mkondo wake huku 

akisisitiza kutaka fedha iliyoibwa kurudi kwa wananchi kwa 

kuwa tangu fedha hizo zipotee miradi mingi imesimama.


Mkuu wa wilaya ya Mlele 

Alhaji Majid Mwanga amemuelekeza mkurugenzi kuchukua 

hatua kwa watumishi wote waliohusika sambamba na kuiarifu 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa 

(TAKUKURU) pamoja na  Jeshi la Polisi ili hatua za 

kuwakamata waliohusika wote ifanyike.


Tarehe 3 Novemba 2023 Mkurugenzi mtendaji wa 

halmashauri ya Mpimbwe alielekeza ufanyike ukaguzi wa 

mapato na matumizi ya kijiji cha Kibaoni ikiwa ni pamoja na 

kuhakiki hoja zilizoibuliwa kwenye taarifa ya Kamati huru ya 

uchunguzi wa migogoro ya ardhi kijiji cha kibaoni ambapo 

kazi ya ukaguzi ilianza 9 Novemba 2023 na kukamilika 

25/3/2024. Miongoni mwa mambo yaliyobainika ni kuwepo 

kwa ubadhilifu wa fedha za umma na matumizi mabaya ya 

madaraka yaliyosababisha baadhi ya viongozi wa kata, 

viongozi na wajumbe wa serikali ya kijiji kuwa ni pamoja na 

watumishi kujinufaisha kwa kujigawia viwanja bila kufuata 

taratibu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.