Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa Ameongoza Kikao Kazi cha Mawaziri na Naibu Mawaziri

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko  alipowasili kwenye viwanja vya jengo la Hazina jijini Dodoma  kuongoza kikao kazi cha Mawaziri, Mei 07, 2024. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Jenista Mhagama na wa pili kulia  ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Dkt. Jim Yonazi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoongoza kikao kazi cha Mawaziri na Naibu Mawaziri  kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 7, 2024. Kushoto ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Jenista Mhagama.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.