Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akitoa maelezo wakati wa ziara ya kukagua Ujenzi wa Mradi wa Skuli ya Sekondari ya Makunduchi ya ghorofa ( G+3 ) iliopo Makunduchi Nganaani Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema
Serikali haijaridhishwa na kasi ya Ujenzi unaoendelea wa Skuli ya Sekondari ya
Makunduchi jambo ambalo linarejesha nyuma dhmira ya Dkt. Hussein Mwinyi ya
kuhakikisha anaondoa changamoto zote kwa wananchi ikiwemo ya Elimu kwa
wanafuzi wa Mikoa yote ya Zanzibar.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na
kukagua maendeleo ya ujenzi wa skuli ya Sekondari ya
Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni utekelezaji wa
ahadi yake ya kuitembelea skuli hio kila ifikipo mwisho wa mwezi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali imeshailipa Kampuni ya Fuchs Contraction Limited shiling Bilioni 4.08 ili kuharakisha umalizikaji wa Ujenzi wa Skuli hiyo lakini kasi ya ujenzi bado inasuasua na kupelekea wanafunzi kuendelea kufuata huduma ya elimu maeneo ya mbali na makaazi yao.
Amesema kuwa endapo Mkandarasi kutoka kampuni ya Fuchs atashindwa
kumaliza ujenzi wa skuli hio na nyenginezo amabazo zinajengwa na kampuni hio
kwa wakati ambao wamekubaliana katika mkataba wao itakuwa wamejinyima
fursa ya kufanya kazi ndani ya Zanzibar hasa katika kipindi cha Serikali ya Awamu
ya Nane(8) na serikali haitalifumbia macho jambo hili.
Amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Nane(8) inayoongozwa na Rais Dkt
Hussen Ali Mwinyi ni kuondoa changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi
ikiwa ni pamoja na kuwekeza zaidi katika Sekta ya elimu ambayo ndio muhimili
mkuu wa maendeleo nchini.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefika katika skuli ya
Sekondari ya Hasnuu Makame kukagua maendeleo ya ukarabati wa
jengo la dahalia ya wanawake liloungua moto na kusababisha hasara kubwa kwa
wanfunzi wanaosoma skulini hapo, na kuwataka walimu na wanafunzi kuendelea
kulitunza na kudumisha usafi ndani na nje ya jengo hilo ili liweze kudumu na
kutumika kwa muda mrefu kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Mhe. Hemed ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Elimu kuhakikisha ndani ya muda
mfupi ujao wanaijengea uzio skuli hio ili kuimarisha ulinzi na usalama kwa
wanafunzi wanaishi hapo sambamba na kumtaka Mkandarasi kutoka Kampuni ya
Faster kuhakikisha anamalizia matengenezo madogo madogo yaliyobakia ndani ya
siku tano(5) ili wanafunzi waweze kuhamia na kuendelea na masomo yao katika
hali ya utulivu.
Nae Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulghulam
Hussein amesema wizara imejipanga kuhakikisha inaipatia kila skuli vifaa vya
kusomea vya kisasa ili kuboresha mfumo wa
elimu Visiwani ZanzibarambapoWizara imefanya ununuzi wa vifaa mbali mbali
ikiwemo vitanda zaidi ya elfu moja(1000) kwa ajili ya skuli ambazo zinamadahalia
Kompyuta, Projecta, viti na meza ambavyo vyote vitagawiwa kwa skuli zote za
Unguja na Pemba.
Mhe. Gulam ameiomba Serikali kuichukulia hatua ya kuipiga penalt Kampuni ya
Fuchs kwa kusababisha kuchelewa kumalizika kwa Ujenzi wa Skuli nane (8)
zinazojengwa na kampuni hio jambo ambalo litatoa fundisho kwa kampuni
nyengine zitakazopatiwa fursa ya kufanya kazi na Serikali ya Awamu ya Nane (8).
Kwa upande wake Mkandarasi kutoka kampuni ya Fuchs Contraction Ltd Devid
Mwasomola amesema changamoto kubwa iliosababisha kishindwa kuendelea na
Ujenzi wa Skuli hio ni kukosekana kwa nondo na malipo kwa ajii ya wafanyakazi
hivyo ameaahidi kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi hio ndani ya
muda uliopangwa kwa sasa.
Katika ziara hio Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametembelea ujezi wa skuli
ya ghorofa (G+3) ya Sekondari ya Makunduchi inayojengwa na Kampuni Fuchs
Contraction Limited, na kukagua maendeleo ya ukarabati wa jengo la dahalia ya
wanawake katika Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame liloungua moto na
kusababisha athari kubwa kwa wanafunzi wanaoishi hapo mwishoni mwa mwaka
jana.
Imetolewa na kitengo cha Habari ( OMPR)
Leo tarehe 01.07.2024
No comments:
Post a Comment