RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Balozi wa Umoja
wa Ulaya Nchini Tanzania Mhe.Christine Grau (kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yaliyofanyika
katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 21-8-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake
Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Mhe.Christine Grau, mazungumzo hayo yaliyofanyika
katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 21-8-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Balozi wa Umoja
wa Ulaya Nchini Tanzania Mhe.Christine Grau (kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yaliyofanyika
katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 21-8-2024

Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake
Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Mhe.Christine Grau,baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa
Ikulu Jijini Zanzibar leo 21-8-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi wa Umoja wa
Ulaya Nchini Tanzania Mhe.Christine Grau,baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa
Ikulu Jijini Zanzibar leo 21-8-2024.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia
kuweka mkazo zaidi kwenye sekta ya mwani ili kuzalisha bidhaa zenye ubora na
kuzipatia soko la uhakika.
Dk. Mwinyi aliyasema
hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Balozi wa Ulaya nchini, Tanzania,
Christine Grau.
Alisema, asilimia 99
ya wakulima wa zao la mwani Zanzibar ni wanawake, hivyo alimueleza balozi huyo
kuangalia haja ya kuwaungamkono wanawake na wakulima wa mwani nchini hasa kwa
mafunzo na vifaa kisasa ili wazalishe mwani wenye ubora utakaoendana sambamba
soko la uhakika.
Mbali na mambo
mengine ya maendeleo na uwekezaji ikiwemo utalii, Rais Dk. Mwinyi pia
alimueleza Balozi Grau kuwa Uchumi wa Buluu ni sera kuu ya Uchumi wa Zanzibar hivyo
alimueleza kuangalia fursa zinazotokana na sera hiyo.
Pia Rais Dk. Mwinyi
ameupongeza Umoja wa Ulaya kwa ushirikiano mzuri uliopo na Tanzania na kueleza
kuwa wameshirikiana kwa miaka mingu kupitia sekta mbalimbali za maendeleo
ikiwemo, Elimu, maji, afya na miundmbinu.
Kwa upande wake
Balozi Christine Grau amesifu juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
inayoongozwa na Rais Dk. Mwinyi na kueleza kuwa wanafanyakazi kwenye maeneo
mbalimbali iliwemo kushirikiana jamii kupitia serikali za mitaa na taasisi za
kiraia (NGO’s) kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa jamii Unguja
na Pemba.
Ameeleza kupitia
mradi wao wa “Green City” wamesaidia masuala ya Jinsia hasa kuwawezesha
wanawake kwenye Elimu, Uchumi ikiwemo Uvuvi, pamoja na masuala ya uongozi wa
fedha.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment