Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imezindua Mradi wa
Kuandaa Mkakati wa Taifa wa muda mrefu wa kupunguza Uzalishaji wa Gesijoto
ambao utasaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mradi huo utakaotekelezwa nchini Tanzania kwa kipindi cha mwaka
mmoja utasaidia kujenga uwezo wa nchi katika kukabiliana na ongezeko la joto hadi
kufikia chini ya nyuzijoto 15.
Akizungumza wakati wa kikao cha uzinduzi wa mradi huo jijini
Dodoma Agosti 26, 2024, Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais
Bw. Abdallah Hassan Mitawi amesema mkakati huo unatarajiwa kuandaliwa ni muhimu
kujumuisha mambo muhimu ya kitaifa.
Amewataka wadau kutoka sekta mbalimbali zinazoshiriki katika
maandalizi yake kuongeza ufanisi wa nishati zinazotumiwa na jamii ambazo ni
safi zisizochafua mazingira ambazo Tanzania imejiwekea lengo kuwa asilimia 80
wananchi watatumia nishati safi ifikapo mwaka 2030.
Halikadhalika, Naibu Katibu Mkuu Mitawi amesema nishati
inayotumika viwandani nayo inapaswa kuangaliwa kwani inaposambaa angani
husababisha ongezeko la joto ambalo ni chanzo cha mabadiliko ya tabianchi.
Ameongeza kuwa kwa vile eneo la usafiri linaweza kusadia katika
kupunguza gesi joto ambalo ambapo kwa sasa tayari Serikali imeanzisha mradi wa
reli ya kisasa (SGR) na mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (DART) hivyo kuwe
na mkakati wa kuitekeleza katika maeneo mengine ya nchi.
Amesema ni wakati sasa mkakati huo ujumuishe namna ya kufanya
biashara ya kaboni na fursa zake pamoja na upandaji wa miti na kuitunza huku
akipongeza Zanzibar kwa kuja na kampeni ya kukijanisha visiwa hivyo.
Awali
akizungumza, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi
Catherine Bamwenzaki amesema lengo la mradi huo kuandaa mkakati wa kukabiliana
na gesijoto kulingana na kifungu
cha 4 (19) cha Makubaliano ya Paris kinachotoa masharti kwa Wanachama kuunda na
kuwasiliana Mikakati ya Muda Mrefu ya Uzalishaji wa Uzalishaji wa gesi chafu,
kwa kuzingatia Kifungu cha 2.
Pia, amesema kikao hicho kilichowakutanisha washiriki 50 kutoka
sekta mbalimbali za Serikali na binafsi kimelenga kutoa taarifa kwa wadau
kuhusu namna ya kutekeleza mradi huo ulioandaliwa katika kipindi cha miaka mitatu
kabla ya kuanza utekelezaji wake
Naye Bi. Viktoria
Dimitrova, kutoka Asasi ya 2050 Pathways Platform amesema mbali
ya Tanzania pia ni nchi zilizonufaika ni pamoja na Pakstan, Rwanda, Jamaica na Senegal.
Amesema katika utekelezaji wa miradi hii ni muhimu kushirikiana na Serikali katika kuandaa mipango madhubuti ya muda mrefu katika kukabiliana na gesijoto.
Mradi huo unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, ufadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kupitia taasisi yake ya Internation Climate Initiative (IKI) na kusimamiwa na Asasi ya 2050 Pathways Platform.
No comments:
Post a Comment