Na Rahma Khamis Maelezo 18/10/2024
Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni Zanzibar, limezuia upigaji wa muziki katika baa zote za Zanzibar ambazo hazina sehemu maalumu ya kuzuia sauti (saund proof) ili kuepusha usumbufu kwa jamii.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari , Katibu Mtedaji wa Baraza hilo Chum Juma Chum, amesema hatua hiyo imekuja baada ya kupata maalamiko kutoka kwa jamii juu ya upigwaji huo wa muziki na kusababisha kero.
Amefahamisha kuwa baraza limesitisha utoaji wa leseni za muziki kwa kumbi za baa hadi pale zitakapokidhi vigezo na masharti ikiwemo sehemu ya kudhibiti sauti.
Hata hivyo baraza linaendelea kufanya ziara ya ukaguzi katika maeneo yote ya kumbi za burudani kwa lengo la kudhibiti athari zinazotokana na kelele za muziki kwa jamii.
Hivyo alizitaka taasisi najamii kwa ujumla kufuata sheria na taratibu za baraza hilo ikiwemo ukataji wa leseni ili kuepusha kufungiwa na endapo watakiuka sheria hizo hatua kali za kisheria atachukuliwa dhidi yao.
Akizungumzia kuhusu Shughuli za kijamii amesema utaratibu utaendelea kama kawaida kwa kufuata maelekezo ya vibali vinavyotolewa na masheha wa maeneo husika.
No comments:
Post a Comment