Naibu Katibu Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Khamis Suleiman Mwalim (Shibu) akifunguwa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na ufahamu wa vyama vya Ushirika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Mapato Ofisi ya Zanzibar Mayungwani Wilaya ya Mjini, na (kulia kwake) Mkurugenzi wa Idara ya Vyama vya Ushirika Zanzibar Khamis Daudi Simba.
Takdir Ali. Maelezo Zanzibar. 04.11.2024.
Waandishi wa habari wametakiwa kuielimisha jaimii juu ya umuhimu wa kuwepo vyama vya ushirika hapa nchini.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Khamis Suleiman Mwalim (Shibu) katika Mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na ushirika huko katika Ukumbi wa Mamlaka ya Mapato Ofisi ya Zanzibar Mayungwani Wilaya ya Mjini.
Amesema sekta ya Ushirika ni muhimu sana kwa kuwaunganisha Wananchi kiuchumi na kuwaletea maendeleo hivyo iwapo Waandishi hao watatumia kalamu zao vizuri wataweza kuisaidia jamii.
Aidha amewataka Wanajamii kuacha kukaa vijiweni kwa madai ya kuwa hakuna ajira na kuwaomba kujiunga katika Sacos ili kupata fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mikopo na mafunzo.
Amebainisha kuwa vyama vya Ushirikia vinasaidia kujenga Uchumi wa nchi kwani kuna wananchi wengi wanaoendesha Maisha yao kupitia vyama vya Ushirika.
Kwa uapande wake Mkurugenzi wa Idara ya Vyama vya Ushirika Zanzibar Khamis Daudi Simba amewataka Viongozi na Wanachama wa Sacos Nchini kufuata misingi ya Ushirika ikiwa ni pamoja na Uwazi, Uwajibikaji, kutoa Mafunzo, Ripoti na kuijali jamii.
Aidha amesema licha ya mafanikio mbalimbali iliopata idara hiyo kama vile kupata Idadi kubwa ya vikundi vya Ushirika lakini wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo uhaba wa Wafanyakazi, Vitendea kazi na Uelewa mdogo kwa baadhi ya Wanajamii juu ya Dhana ya Vyama vya Ushirika.
Nae Afisa wa maendeleo ya vyama vya Ushirika Zanzibar Zainab Abulkadir amesema maafisa ushirika wa Wilaya wanafanya ukaguzi kwa kila baada ya miezi mitatu kwa kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo Wanachama, Fedha, mikopo na Mafunzo.
Hata hivyo amesema idadi ya migogoro imepunguwa kutokana na mikakati Madhubuti iliowekwa na Idara hiyo sambamba na kuwaomba Wananchi kufuata taratibu na Sheria zilizowekwa na vyama vya Ushirika ili kuepukana migogoro inayoweza kuepukika.
Nao Waandishi wa habari walioshirikiki katika Mafunzo hayo wameipongeza Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji kupitia Idara ya Maendeleo ya vyama vya Ushirika kwa kuweka mikakati ya kutoa elimu kwa Waandishi wa Habari jambo limeweza kutoa uelewa wa masuala hayo.
No comments:
Post a Comment