Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Mhe Dk. Hussein Ali Mwinyi Amekwenda Nchini Zimbabwe Kuhudhuria Mkutano wa SADC.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na  Mkewe Mama Mariam Mwinyi akisalimia na  kuagana na Viongozi mbalimbali wa Serikali, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo 19-11-2024, akielekea Nchini Zimbabwe kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC, akimuwakilisha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, utakaofanyika tarehe 20 Novemba 2024, jijini Harare, Zimbabwe.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na  Mkewe Mama Mariam Mwinyi akisalimia na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdalla, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo 19-11-2024, akielekea Nchini Zimbabwe kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC, akimuwakilisha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, utakaofanyika tarehe 20 Novemba 2024, jijini Harare, Zimbabwe.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.