Habari za Punde

Tume yawanoa Ma-OCD’s nchini kuhusu sharia za uchaguzi

Na Mwandishi wetu, Kilimanjaro

Tume Huriu ya Taifa ya Uchaguzi katika kuhakikisha ionatoa Elimu ya Mpiga Kura kwa makundi mbalimbali katika jamii, leo Novemba 07, 2024 imetoa elimu hiyo kwa Wakuu wa Polisi Wilaya (OCD) nchini katika mafunzo yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

 

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo ya siku moja kuhusu Sheria mbalimbali na Kanuni zinazoiongoza Tume, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani amesema kwa kuwapa elimu hiyo maafisa hao wa Polisi ngazi ya Wilaya kutasaidia kuondoa migongano baina yao na Vyama vya siasa.

 

“Kimsingi hawa ndio wasimamizi wa sheria ngazi ya Wilaya kutoka Jeshi la Polisi, hivyo tumewapitisha katika Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Sheria ya Rais, Wabunge na Madiwani ili iwawezeshe kuzitafsiri vyema hizi sheria na zitawawezesha katika usimamizi bora wa majukumu yao bila kuleta mtafaruku kati ya chama cha siasa au na wanachi kiujumla,” alisema Bw. Kailima.

 

Kailima amesema kwa sasa Polisi wanajua Wajibu wao ni nini na chama cha siasa kinatakiwa kufanya nini wakati huu ambapo Tume inaendelea na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini.

 

Aidha, Kailima amesema wakati wa kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, Tume itakutana tena na Jeshi hilo na kuwapa ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yahusuyo Uchaguzi Mkuu ili kuendelea kuwa na uchaguzi mkuu wa amani, huru na haki na kuwezesha baada ya uchaguzi Mkuu hali inaendelea kuwa ya utulivu.

 

Kwa upoande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, CP Awadhi Juma Haji amesema lengo la mafunzo hayo ni kuliweka tayari Jeshi la Polisi wakati wa mchakato wa uchaguzi na kwakuzingatia kua wao ndio wasimamizi wa sharia na walinzi wa raia na mali zao wakati wote.

 

CP Awadh amesema Tume imewapa elimu juu ya wajibu wa Polisi katika shughuli za uchaguzi, sheria na kanuni mbalimbali wakati huu wa uboreshaji na lengo ni kujipanga na kuhakikisha mazoezi yanayoendelea nchini yanafanyika katika hali ya usalama mkubwa.

 

Mafunzo hayo ya siku nne ya Wakuu wa Polisi Wilaya Nchini yaliyoanza Novemba 4, 2024 yanataraji kufikia tamati Novemba 8 mwaka huu ambapo mada mbalimbali kuhusu uchaguzi na ushiriki wa jeshi la Polisi zimetolewa.

 

MWISHO. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.