Habari za Punde

WAZIRI CHANA AWATAKA WATANZANIA KUWAENZI MASHUJAA

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) akiweka shada la maua katika Makaburi ya Jumuiya ya Madola katika Siku ya Kumbukumbu ya  Mashujaa waliopigania Vita ya Kwanza ya Dunia iliyofanyika jijini Dar es Salaam Novemba 10,2024.

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Watanzania kuwaenzi mashujaa kwa  kuendeleza utu, amani na ubinadamu walioupigania ili kuifanya dunia kuwa mahali salama pa kuishi.

Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa mgeni rasmi katika Siku ya Kumbukumbu ya  Mashujaa waliopigania Vita ya Kwanza ya Dunia iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 10,2024.

Katika Siku hii ya Kumbukumbu, sio tu kwamba tunaadhimisha maisha yao bali tunafanya upya dhamira yetu ya kushikilia kanuni walizozisimamia, ambazo ni dunia yenye amani, ubinadamu na utu” Mhe. Chana amesisitiza.

Amefafanua kuwa katika kumbukumbu za mashujaa hao, jamii zinahimizwa kulinda amani waliyoipigania kwa ujasiri, na kuendeleza urithi wao kwa kujenga madaraja ya maelewano na ushirikiano kuvuka mipaka ya nchi na kusisitiza kuwa pamoja na changamoto mbalimbali za amani duniani, Tanzania imesimamia imani yake kwamba suluhu za migogoro ya kudumu hazitokani na mtutu wa bunduki bali kupitia diplomasia, mazungumzo na maelewano.

Aidha, ameongeza kuwa zinahitajika juhudi za pamoja ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za kidunia kama mabadiliko ya tabia nchi, umaskini, ukosefu wa chakula, magonjwa ya milipuko na ukosefu wa usalama mtandaoni, kuhakikisha kwamba vizazi vijavyo vinarithi ulimwengu ambao sio tu wa amani bali uthabiti na wa haki.

Mhe. Chana ametumia fursa hiyo kuziomba Jumuiya za Kimataifa kuzidisha juhudi za kuleta maazimio ya amani huku akiwapongeza mashujaa waliojitolea kudumisha amani.

Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani na Ubalozi wa Uingereza nchini, yamehudhuriwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Thomas Terstegen, Mwakilishi wa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo Ubalozi wa Uingereza, Kemi Williams, Waheshimiwa Mabalozi na Makamishna Wakuu, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na Maafisa wa Serikali.

 

Brass band ikitumbuiza katika Siku ya Kumbukumbu ya  Mashujaa waliopigania Vita ya Kwanza ya Dunia iliyofanyika jijini Dar es Salaam Novemba 10,2024.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) (katikati), Mwakilishi wa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo Ubalozi wa Uingereza, Kemi Williams (kushoto) na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Thomas Terstegen katika Siku ya Kumbukumbu ya  Mashujaa waliopigania Vita ya Kwanza ya Dunia iliyofanyika jijini Dar es Salaam Novemba 10,2024.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) akizungumza katika Siku ya Kumbukumbu ya  Mashujaa waliopigania Vita ya Kwanza ya Dunia iliyofanyika jijini Dar es Salaam Novemba 10,2024.

Baadhi ya washiriki wa Siku ya Kumbukumbu ya  Mashujaa waliopigania Vita ya Kwanza ya Dunia wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb)(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza ) akizungumza katika Siku ya Kumbukumbu ya  Mashujaa waliopigania Vita ya Kwanza ya Dunia iliyofanyika jijini Dar es Salaam Novemba 10,2024.

3





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.