Habari za Punde

DKT. NCHEMBA AHITIMISHA ZIARA NCHINI OMAN

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akipokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Fatma Rajab, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muscat – Oman, baada ya Mhe. Dkt. Nchemba kuhitimisha ziara ya kikazi nchini humo.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza katika kikao kifupi baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Fatma Rajab, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muscat – Oman, baada ya Mhe. Dkt. Nchemba kuhitimisha ziara ya kikazi nchini humo.

Na Saidina Msangi, WF, Muscat, Oman

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Oman ambapo akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muscat – Oman, akielekea nchini Saudi Arabia ambako atakuwa na ziara nyingine ya kikazi, aliagwa na Mhe. Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Fatma Rajab.

Akiwa nchini Oman, pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba alitia saini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi, ujulikanao kama An Agreement for the Elimination of Double Taxation with Respect to Taxes on Income and Prevention of Tax Avoidance and Evasion, wenye lengo la kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.

Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba, amewasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kushiriki katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji, linalotarajiwa kufanyika katika Makao Makuu ya Chemba ya Biashara Riyadh, Saudi Arabia.

Mwisho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.