Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. Ali Suleiman Amefungua Barabara ya Donge - Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja Shamrashamra za Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais IkuluAli Suleiman Ameir  kulia akikunjuwa Kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika Uzinduzi wa Barabara za Donge -Chaani na za karibu yake 15.7 km Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu :Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.

Na.Rahma Khamis Maelezo. 31/12/2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. Ali Suleiman Ameir amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na mipango bora ya kujenga barabara zote kwa kiwango Cha lami Mjini na Vijijini.

Ameyasema hayo Donge Wilaya ya Kaskazini B' Unguja katika ufunguzi wa barabara ya Donge_Chaani  yenye urefu wa kilomita 15.7 ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za kutimiza miaka 61 ya Mapinduzi.

Aidha amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha barabara kuu na za ndani zinajengwa kwa lami na kupitika muda wote

Amesema kuwa  kukamilika kwa Barabara hizo. ni chachu ya kukuza Uchumi na Sekta nyengine ikiwemo Uvuvi, Kilimo, Utalii  pamoja na Biashara.

Katika hatua nyengine Waziri Mrembo amewataka wananchi ambao bado hawajajengewa barabara zao kwa kiwango Cha lami kuwa wastahamilivu kwani barabara hizo zitakengwa kwa muda mfupi ujao.

Akitoa taarifa ya kitaalamu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Makame Machano Haji amesema kuwa barabara hiyo ina uwezo wa kudumu kwa muda wa miaka 25 Hadi 30 na imezingatia miundombinu yote muhimum ikiwemo njia za kupitishwa Maji ya mvua pamoja na daraja.

Aidha amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya chama Cha Mapinduzi katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma Bora muhimu.

Nao wananchi wa maeneo hayo wamesema kuwa barabara hiyo ni msaada mkubwa kwao kwani itafungua fursa za kiuchumi kupitia harakati zao za kiuchumi na kimawndeleo

Ujenzi wa barabara hiyo ni muunganisho wa barabara za Donge Mbiji, Donge Mchangani, Donge Chechele na Mkwajuni Donge ambazo zinakadiriwa kufikia Dola za Kimarekani Milioni 7.323 Hadi kukamilika kwake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Ali Suleiman Ameir  katikati akikata Utepe kuashiria  Uzinduzi wa Barabara za Donge -Chaani na za karibu yake 15.7 km Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu :Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais IkuluAli Suleiman Ameir  katikati akiwa pamoja na Viongozi wengine wakitembea kwa miguu baada ya  Uzinduzi wa Barabara za Donge -Chaani na za karibu yake 15.7 km Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu :Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.
 Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiendesha Pikipiki kuonesha kumpokea Mgeni Rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Barabara za Donge -Chaani na za karibu yake 15.7 km Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu :Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Makame Machano Haji akutoa maelezo ya Kitaalamu katika hafla ya Uzinduzi wa Barabara za Donge -Chaani na za karibu yake 15.7 km Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu :Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Ali Suleiman Ameir akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Barabara za Donge -Chaani na za karibu yake 15.7 km Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu :Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika hafla ya Uzinduzi wa Barabara za Donge -Chaani na za karibu yake 15.7 km Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu :Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.
Picha na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar ,31/12/2024

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.