Habari za Punde

Vijana Kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kupoteza muelekeo wa ndoto za maisha.

Mwakilishi wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Magharibi 'Kichama Mhe.Fatma Ramadhani Mandoba akikabidhi msaada wa kwa Kikundi cha Kiembeni Group kwa kiongozi wa kikundi hicho  Ali Mbaraka  Faki akipokea fedha hizo, hafla hiyo iliyofanyika Fuoni Migombani Wilaya ya Magharibi 'B' Unguja.
Baadhi ya wanakikundi wakimsikiliza Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi 'Kichama Mhe.Fatma Ramadhani (hayupo pichani) huko Fuoni Migombani  Wilaya ya Magharibi 'B'.

Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi 'Kichama Mhe. Fatma Ramadhan Mandoba amewataka Vijana Kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kupoteza muelekeo wa ndoto za maisha.

Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kuhamasisha vikundi vya Ujasiriamali huko Fuoni Migombani Wilaya ya Magharibi "B".

Amesema kuna vishawishi vingi vinavyoweza kupelekea Vijana kupoteza muelekeo wa maisha yao ikiwemo Utumiaji wa Dawa za kulevya, Bangi na Uhasharati.

Aidha amewapongeza Vijana kwa hatua walioichukuwa ya kuanzisha  Vikundi vya Ujasiliamali jambo ambalo litasaidia kujipatia kipato cha kuendeysha maisha yao ya siku. 

Hata hivyo amewataka Vijana hao kujitokeza kwa wingi katika Daftari la kudumu la wapg kura awamu ya pili wakati utakapofika ili kupata haki yao ya kuchaguwa na kuchaguliwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Dimani kichama  Zuhura  Suleiman Ali  amewataka Vijana hao kuvisajili vikinfi vyao ili waweze kupatiwa fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo elimu na mikopo.

 "Iwapo vikundi vyetu hatuta visajili na kupata nambari za Benki vikundi vyetu havitopata mikopo hata siku moja" alisema Mwenyekiti.

Nae Mshika fedha wa kikundi cha Dira ya Mafanikio Asia Abdalla Ibrahim na  Ali Mbaraka Faki wamwsema wanachangamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa Mitaji, Ofisi na vitendea kazi ikiwemo compyuta na mashine ya Fotokopi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.