Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)(kulia), akiagana na Balozi wa Japan nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe.Yasushi Misawa, baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba alimhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania na Japan zitaendelea kuimarisha uhusiano wake wa kiuchumi na kijamii kwa faida ya nchi hizo mbili huku Mhe. Balozi Misawa kwa upande wake, akisema Tanzazania na Japani zina uhusiano wa kihistoria ambao nchi yake itauendeleza kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na nchi yake.
Labels
- .
- `
- 8
- AFYA
- AFYA.
- AJALI
- BIASHARA
- BURUDANI
- DINI
- ELIMU
- FILAMU
- HABARI
- HARUSI
- HOSPITALI
- I
- JAMII
- KATUNI
- Kii
- KILIMO
- KIMATAIFA
- KITAIFA
- Ku
- MAGAZETI
- Mahkamani
- MAISHA
- MAKALA
- MAKALA AFYA.
- MAKALA.
- MATUKIO
- MATUKIO.
- MICHEZO
- MITAANI
- MIUNDOMBINU
- MSAADA
- Ok
- SIASA
- TANGAZO
- TAWA YAWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI
- TEKNOLOJIA
- UCHUMI
- UTAFITI
- UTALII
- VIDEO
- VIJANA
- VISA INTERNATIONAL YAZINDUA TAWI TANZANIANa Mwandishi wetu 16.07.2025DAR ES SALAAM
- WEZI
Tafsiri ya Lugha
Popular Posts
- 
Mtaalamu wa lugha ya Alama Masika Khamis Ali akitoma maelezo kwa Wananchi wa makundi maalumu wakati wa ufungaji wa Mkutano wa Kampeni wa Cha...
- 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Ujumbe wa Misheni ya Uangalizi wa Uch...
- 
Dar es Salaam. 28-10-2025 Tanzania Bloggers Network (TBN) inatoa pongezi za dhati kwa Watanzania wote, wagombea, vyama vya siasa, Tume Huru ...
- 
Na Mwandishi Wetu WMJJWM- Njombe Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Mkaundi Maaalum Dkt. John Jingu, amewataka...
- 
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Bernard Marce...
- 
Msanii wa Bongo Fleva Nandy akiburudisha kwa wimbo wake wa kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein A...
- 
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kutokuwa na hofu ya ulinzi na usalama wao siku ya uchaguzi Oktoba 29, 2025 na limewasihi wakapige kura n...
- 
Shamrashamra za ufungaji wa mkutano ya Kampeni wa Chama Cha Mapiduzi (CCM) za Ubunge,Uwakilishi na Udiwani Jimbo la Chumbuni Zanzibar , kwa ...
- 
Shamra shamra wakati akiwasili Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa...
DKT. NCHEMBA AMUAGA BALOZI WA JAPAN NCHINI. AWAALIKA WAWEKEZAJI KUTOKA JAPAN
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WF, Dodoma)
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ametoa wito kwa Kampuni za Japan kuwekeza nchini Tanzania ili kutumia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali za uzalishaji kwa faida ya pande zote mbili.
Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo Jijini Dodoma wakati akiagana na  Balozi wa Japan nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe.Yasushi Misawa, ambapo pamoja na mambo mengine, alimhakikishia pia Balozi huyo kuwa Tanzania na Japan zitaendelea kuimarisha uhusiano wake wa kiuchumi na kijamii kwa faida ya nchi hizo mbili.
Alisisitiza kuwa Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji ikiwemo sekta ya kilimo itakayoiwezesha Tanzania kuwa ghala la chakula lakini pia uwekezaji katika miundombinu ikiwemo uendeshaji wa Reli ya Kisasa SGR.
Aidha, katika mazungumzo yao, Dkt. Nchemba aliishukuru Japan kwa uwekezaji mkubwa uliochangia maendeleo ya nchi kupitia miradi mbalimbali iliyofadhiliwa na nchi hiyo katika sekta za kilimo, afya, nishati, na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo Barabara ya mzunguko katika jiji la Dodoma.
“Katika kipindi chako pekee, tumeshuhudia Tanzania na Japan zikisaini mikataba ya mikopo nafuu yenye thamani ya yen ya Japan bilioni 10 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 151 pamoja na msaada wa yen bilioni 5.5, sawa na zaidi ya shilingi za Tanzania bilioni 83. Tunakushukuru sana na tunakuomba uendelee kuwa Balozi mzuri wa Tanzania hata baada ya kumaliza muda wako” Alisisitiza Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa, aliyeambatana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Ara Hitoshi, alisema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na nchi yake umedumu kwa zaidi ya miaka 60 ambapo katika kipindi hicho, Japan imesaidia utekelezaji wa zaidi ya miradi 360 ya kijamii na kiuchumi.
Alibainisha kuwa baadhi ya miradi hiyo iko katika sekta ya nishati ukiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa njia ya umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga, ujenzi wa mradi wa umeme unaounganisha Tanzania na Kenya pamoja na mpango unaoendelea kati ya Tanzania na Japan kupitia Wizara ya Nishati wa kujenga mradi wa umeme wa joto ardhi.
Katika mazungumzo yao ambayo yalihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, viongozi hao walijadili fursa mbalimbali za maendeleo katika sekta za kilimo, afya, miundombinu, na kukuza uchumi na maendeleo ya nchi kupitia ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi pamoja na uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
BLOGU RAFIKI
- 
- 
Rais na Mgombea wa nafasi ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan apiga Kura katika Kituo cha Ofisi ya Kijiji Chamwino mkoani Dodoma - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) M...2 days ago
- 
Elimu : Bajeti za Elimu Zisipuuzwe wakati wa misukosuko ya Kiuchumi na Kisiasa Duniani - Kikwete na Malala Waonya. - Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Malala Yousafzai, wameonya juu ya mwenendo hatarishi duniani wa kupunguza au ku...2 weeks ago
- 
MAHOJIANO YA TAUSI SUEDI NA AMRI NGOYE KUHUSU CSI KUPITIA KWANZA PRODUCTION NCHINI MAREKANI - Pata habari motomoto kupitia facebook kwa kulike huu ukurasa wetu https://www.facebook.com/pages/Pamojapureblogspotcom/312633955485619?ref=hl7 years ago
Marafiki Duniani
Popular Posts
- 
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili Zanzibar majira ya mchana kwa Ndege na kuendelea na taratibu za Maziko yatafanyika katika Mtaa wa...
- 
The United Republic Of Tanzania National Examination Council of Tanzania Form Four Examination Results 2017/2018 The National E...
- 
Makamanda wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Waziri Kiongozi wa Kwanza wa Zanzibar na Brigedia Jenerali Mstaaf Ramadhani Haji Faki...
- 
Na Miza Kona/Rahma Khamis Maelezo-Zanzibar Jumla ya wanafunzi 16,744 wamechaguliwa kuendelea masomo ya kidatu cha tatu kati ya wanafun...
- 
Bwana Harusi Lusajo Sajent Mwangambaku (kushoto), akiwa katika pozi na mke wake Neema Stanley Matowe katika hafla yake ya ndoa iliyofa...
- 
Mama mjazito akihangaika na hatimaye kupoteza maisha kutokana na mimba za utotoni..Video ipo hapo chini baada ya maelezo mafupi
- 
Hutuba ya Mhe Waziri wa Afya Nd. Mahmoud Thabit Kombo kwa Waandishi wa Habari Katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Dunia Zanzibar, 22...
- 
Madawa na Maji vilivyokabidhiwa na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya Kambi za K...
 

 
.jpeg) 
 
 
 
 
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment