Habari za Punde

Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe.Othman Masoud Akizungumza na Ujumbe wa Kamati ya Kupambana na Udhalilishaji Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Januari 08 2025, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Kamati ya Kupambana na Udhalilishaji Zanzibar.

Ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wake,  ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, Bi. Mwanamkaa Abdulrahman Mohammed, umefika Ofisini kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kwaajili  ya kuwasilisha Taarifa ya Mwenendo wa Udhalilishaji Nchini, pamoja na kupata  ushauri kutoka kwa Mheshimiwa Othman.

Ujumbe aliofuatana nao Bi. Mwanamkaa, umewajumuisha pia Maafisa kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, wakiwemo Bw. Mohamed Kassim Hassan na Ostadh Abdulkarim Said Abdulla. 



Kitengo cha Habari

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Januari 08, 2025.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.