Habari za Punde

Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Yalaani Mauaji ya Kimara Dar es Salaam

Na.Mwashaja Juma. THBUB. 

Tume ya Haki za Binaadam na Utawala Bora (THBUB) imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Bw. Jumaanne Juma (28) aliyekuwa mkaazi wa mtaa wa Kimara B, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam aliyeuawa kwa kuchomwa na mafuta ya petrol na watu aliokuwa akiwafanyia kazi za nyumbani kwa madai ya kuwaibia kiasi cha shilingi 200,000.

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi na vyombo vya habari zinaeleza kuwa watu waliomuua Bw.Jumanne walimfuata nyumbani kwake majira ya saa 4 usiku kumtaka waondoke naye wakamlipe malipo yake pamoja na kumpatia kazi nyengine. Hata hivyo, baada ya kuondoka naye walimpeleka mahali, wakanunua mafuta ya petroli na kumchoma moto.

Katika ufuatiliaji wake THBUB imebaini yafuatayo:

              i.   Baadhi ya wananchi bado hawashimu Katiba ya Nchi kama inavyoelekeza katika Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na sheria za Nchi na hivyo kujichukulia sheria mikononi.

      ii. Vitendo vya mauaji vinavyotokea hivi karibuni vimeambatana na ukatili dhidi ya ubinaadamu na

                 iii.     Kuna viashiria vya wananchi kutokuwa na imani na vyombo vya usimamizi wa haki.

Kutokana na tukio hilo ambalo limesababisha kifo cha Bw. 

Jumanne juma,  THBUB inapenda kutamka kuwa kitendo 

hicho ni :

                 i.     Ukiukwaji wa  haki ya kuishi kama ilivyotamkwa katika Ibara ya 14 Katiba  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na hivyo inalaani vikali vitendo hivyo; na

    ii.        Ukatili dhidi ya binaadamu ambao ni kinyume na Ibara ya 13(6)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

THBUB inatambua jitihada za zilizofanywa na Jeshi la Polisi kwa kuwakamata watuhumiwa. Pamoja na hayo, THBUB inapendekeza yafuatayo:

1.    Jeshi la Polisi Tanzania

§  Liendelee kuchukua hatua mahsusi kuimarisha ulinzi katika maeneo ya wananchi na kuwezesha  kuapata taarifa za mapema kuhusu kuwepo viashiria vya uvunjifu wa sheria ikiwa ni pamoja na mauaji na vitendo vya ukatili.

§  Liimarishe ulinzi shirikishi kupitia vituo vya Polisi kata kwa kuongeza idadi ya vituo na idadi ya askari ili kuongeza ufanisi. 

2.    Serikali za Mitaa

§  Mamlaka za Serikali za Mitaa katika ngazi zote ziwe na mipango madhubuti ya kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.§   

3.   Viongozi wa Dini

§  Waongeze nguvu katika utoaji wa elimu ya dini na maadili na kukemea uovu unaotokea nchini. 

4.   Wananchi

§  Wajenge utamaduni wa kuheshimu sheria za nchi, haki za binaadamu, kufuata namna bora ya kupata suluhu ya migogoro na kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi.

§  Washirikiane na vyombo vya dola kufichua maovu kwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili kuzuia matukio kama hayokutokea. 

5.   Asasi za Kiraia na vyombo vya Habari 

§  Kuendelea kutoa taarifa za matukio ya uhalifu kwa wakati na kushiriki kwa ukamilifu katika kutoa  elimu kwa umma kuhusu taratibu zilizopo za namna ya kushuhulikia masuala mbalimbali ya kijamiikupitia sheria na hivyo kulinda haki za binaadamu na utu wa mtu. 

THBUB inatoa pole kwa ndugu, jamaa na wanafamilia waliopoteza mpendwa wao katika tukio hili na inaahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika jitihada za kukomesha na kulinda haki za binaadamu na misingi ya Utawala Bora

Jukumu la ulinzi na utetezi wa haki za binaadamu ni letu sote! 

Imetolewa na:

Mathew P.M. Mwaimu (Jaji Mstaafu)

MWENYEKITI

TUME YA HAKI ZA BINAADAMU NA UTAWALA BORA. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.