Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais
Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali bungeni jijini Dodoma wakati wa Kikao cha Nne cha Mkutano wa 18 wa Bunge Januari 31, 2025.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema Serikali inaendelea na tathmni ya uwepo wa magugu maji katika Ziwa Victoria ili kupatia ufumbuzi changamoto hiyo.
Mhe.
Khamis ameliarifu Bunge jijini Dodoma leo Januari 31, 2025 wakati akijibu swali
la Mbunge wa Geita Mjini Mhe. Constantine John Kanyasu aliyetaka kujua kama Serikali inafahamu ongezeko la magugu maji katika Ziwa
Victoria, zipi ni athari za magugu hayo na mpango wa kuyadhibiti.
Amesema Serikali imechukua jitihada za kudhibiti magugu
maji katika ziwa hilo ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa na kutekeleza
Mkakati na Mpango Kazi wa Taifa wa Kukabiliana na Viumbe Vamizi wa mwaka
2019-2029 ambao unatoa mwongozo wa namna ya kuzuia kuingia na kuenea kwa viumbe
vamizi na una mipango endelevu ya kushughulikia viumbe vamizi waliopo na wale
wanaoweza kuingia.
“Mheshimiwa Spika, tathmnini inaendelea na nimuombe Mheshimiwa Bunge avute
subira wakati tunaendelea kulishughulikia jambo hili kwani limeendelea kuathiri
vyanzo vingi vya maji nchini kwa mfano Ziwa Jipe nalo lina changamoto ya
kuzingirwa na maji,” amesema Mhe. Khamis.
Ameongeza
kuwa Serikali inawajengea uwezo wananchi wanaoishi karibu na ziwa kuhusu namna
ya kujitolea katika kazi za kutokomeza na kuenea kwa magugu maji kila
yanapojitokeza ikiwemo kung’oa, kukausha na kuchoma magugu maji na kuendelea
kufanya tafiti mbalimbali ili kudhibiti uharibifu mifumo ikolojia ya Ziwa
Victoria.
Katika
hatua nyingine, Naibu Waziri Khamis amesema Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura ya 191
imeweka msisitizo kwa miradi yote mikubwa ni lazima ifanyiwe tathmini ya awali
ya athari za mazingira kabla ya mradi kuanza ili kuepuka uharibifu wa
mazingira.
Amesema
Sheria pia inahimiza wananchi kuhamasishwa kushiriki katika uhifadhi wa
mazingira kupitia elimu, sheria ndogo za serikali za mitaa, na mipango ya
hifadhi ya mazingira.
Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Bahi Mhe. Kenneth Ernest
Nollo aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuweka Sheria Kabambe
kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini.
Amefafanua kuwa Sheria hii imeweka msisitizo wa udhibiti wa uharibifu wa
mazingira kwa kukataza uchafuzi wa maji, hewa, na udongo kupitia kemikali za
viwandani, kilimo, na shughuli nyingine za binadamu.
Halikadhalika, Naibu Waziri
Khamis ameriarifu Bunge kuwa Serikali kupitia Wizara ya Maji imetenga fedha
shilingi bilioni 1.08 kwa ajili ya ukarabati wa Bwawa la Kalemawe lililopo katika Wilaya Same
mkoani Kilimanjaro.
Akijibu swali la Mbunge
wa Viti Maalum Mhe. Naghenjwa
Livingstone Kaboyoka aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuondoa
tope lililojaa katika Bwawa la Kalemawe – Same, Mhe. Khamis amesema ukarabati umepangwa kufanyika katika robo ya
nne ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Ametaja shughuli zinzotarajiwa
kufanyika ni pamja na kukamilisha kazi ya usanifu wa kina na kuandaa gharama
kwa ajili ya ukarabati wa bwawa hilo kwa kuondoa tope, kukarabati utoro wa
maji, kujenga msingi wa tuta na tuta la bwawa.
No comments:
Post a Comment