Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt,Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zina dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo kwa Wananchi kutokana na mageuzi makubwa yanayoendelea kufanyika katika sekta zote za Kiuchumi.
Rais Dkt,Mwinyi ametoa tamko hilo alipozungumza katika hafla ya kupokea Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania kwa Mwaka 2023/2024 hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Verde Mtoni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.
Amefahamisha kuwa ili mageuzi hayo yafanikiwe ni vema Sekta ya Bima iendane na kasi ya Serikali zote mbili kwa kujikita kwenye ubunifu na matumizi ya teknolojia na watoa huduma za Bima na Wadau wote wafanye kazi kwa Weledi na Ushirikiano.
Amefahamisha kuwa ili lengo la kupiga hatua zaidi ya Maendeleo katika Uimarishaji wa Sekta ya Bima ni lazima kuandaliwa Mikakati ya Kukabiliana na Changamoto zinazoikabili Sekta hiyo.
Ameyataja Maeneo ambayo yanayohitaji kuimarishwa kuwa ni pamoja na kuwa na Mchakato wa kuwa na Bodi ya Wataalamu wa Bima, Hifadhi ya Jamii na Actuarials Ukamilishwe haraka ili kuwa na bodi itakayosimamia Wataalamu wa Sekta hiyo.
Amesisitiza kuongezwa jitihada zaidi katika Matumizi ya Tehama,Ubunifu wa bidhaa za Bima na Utoaji wa Elimu ya Bima kwa Wananchi.
Dkt, Mwinyi amesisitiza kufanyika kwa Utafiti kubainisha aina ya Vihatarishi vinavyotakiwa kupewa kinga kupitia Bima kwa Mali za Serikali na Mamlaka ya Bima Ipitie Sheria na Kanuni mbalimbali za Bima ili ziendane na Mazingira ya sasa na Ukuaji wa Uchumi.
Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Kus hirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Itaendelea kuweka Mazingira Wezeshi kwenye soko la Bima ili kuongeza Pato la Taifa kupitia Sekta hiyo.
Dkt,Mwinyi amewasisitiza Wananchi na Wadau kuendelea kutumia huduma za Bima na Mamlaka husika zifanye bidii ya kuhakikisha Nchi inanufaika na Huduma hizo.
Ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania kwa Kuanzisha Ofisi ya TIRA kanda ya Unguja na Ofisi ya Kanda ya Pemba na kusisitiza Kutolewa Elimu zaidi kwa Wananchi ili wapate Uelewa zaidi wa Masuala ya Bima.
No comments:
Post a Comment