Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan akizungumza na kumtambulisha Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, wakati wa mkutano wake wa Kampeni uliyofanyika katika viwanja vya Kagengwa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja leo 17-09-2025.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan akizungumza na kuwatambulisha Wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Ubunge, Uwakilishi na Madiwani wa Mkoa wa Kusini Unguja na kuwaombea Kura, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliyofanyika katika kiwanja cha Kagengwa Makunduchi.
Na.Mwandishi Wetu.
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM Dk.Samia Suluhu Hassan amesema amani, utulivu na mshikamano inatakiwa iendelee kudumu katika kipindi chote Cha uchaguzi mkuu utaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Hayo aliyasema jana, Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja katika mkutano wa kampeni za CCM za uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alisema miaka mitano ijayo wamepanga kutekeleza mambo mbali mbali yaliyokuweno katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025/2030 Kwa Zanzibar na Tanzania Kwa ujumla.
Alisema amani, utulivu na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndio tunu za Taifa hili zilizoachwa na waasisi wa nchi , hivyo aliwasihi Watanzania wadumishe amani na utulivu wakati wote katika uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Alifafanua kuwa, tunu amani, utulivu na mshikamano imejengwa sifa Tanzania kimataifa, kikanda na kitaifa Duniani, hivyo lazima ilindwe na kuwatahadharisha wataotaka kuchezea tunu hizo kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri katika kipindi Cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alisema Serikali inachukua jitihada za kuhifadhi Muungano huo, ambapo watafungua kituo Cha kumbukunbu na nyaraka za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili vijana wanaotoka nje wakija nchini waweze kujifunza.
"Suala la utulivu wa kisiasa na amani ya nchi katika kipindi Cha uchaguzi ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na amani na utulivu kama wazee wa Pemba alipokenda kuwatenbelea walimuomba amani na utulivu," alisema.
Alisema uchaguzi sio vita ni kitendo Cha demokrasia, hivyo watu waende kupiga kura na kurudi majumbani kwao Oktoba 29 mwaka huu.
Alisema sio muda wote kushika silaha inaleta amani , hivyo amani na utulivu ndio silaha muhimu katika uchaguzi.
Alieleza sasa ni zamu ya Zanzibar wahenga huwa wanasema sadaka huwa inaanzia nyumbani katika uwanja wa kajengwa kuomba baraka huanza nyumbani ili kuendelea kufanya makubwa zaidi miaka mitano ijayo.
Alisema wametekeleza Kwa mashirika makubwa baina ya Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika sekta mbali mbali za kijamii na kiuchumi
Alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeendelea kudumishwa na kuwaenzi wazee na waasisi wa nchi hii Hayati Nyerere na Mzee Karume tangu mwaka 1964 walipounganisha nchi hizo na kupata mafanikio katika kifamilia, kibiashara, kiuchumi na kisiasa.
Alieleza Muungano umekuwa wa udugu wa damu zaidi pamoja na kulinda uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, pamoja na amani na utulivu ndio tunu za nchi.
Aidha alimshukuru Dk. Mwinyi Kwa Maendeleo makubwa katika miaka mitano iliyopita, ambapo huko nyuma alikuwa anaitwa Mzee wa mabati lakini baadae makasi uliongea katika kukata miradi ya hospital, Masoko, skuli na majengi ya Mahakama .
Alisema ushirikiano mkubwa wa Watanzania wote waliowapa miaka mitano iliyopita aliwaomba wawape kura ili miaka mitano ijayo wawafanyie makubwa zaidi. Alisema CCM lengo lao ni kuwatumikia Watanzania na kujenga taswira ili wasonge mbele.
Nae Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Asha- Rose Migiro wakati akiwatambulisha wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan na Mgombea wa Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi wote wamekuwa wakisisimia amani, Umoja na mshikamano pamoja na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Alisema Leo ni furaha Dk. Samia kupokelewa nyumbani ambapo katika safari hiyo ya kampeni wakati wa uzinduzi ulisisitiza amani, utulivu na mshikamano Kwa ajili ya kujenga Tanzania yenye ustawi wa Jamii na kuwaunganisha Watanzania wote.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Dk. Dimwa alisema mambo matano yamefikiwa na Dk. Samia na Dk. Mwinyi ikiwemo uimarishaji wa uchumi katika kuimarisha miradi ya kimkakati na kutoa ajira Kwa vijana na wanawake.
Alisema kuimarisha miundombinu ya barabara, Bandari, uwanja wa ndege , kuimarishwa Kwa sekta ya afya, kuimarisha diploma ya uchumi, ambayo Tanzania inaheshimika kimataifa na kudumishwa Kwa amani na utulivu nchini.
Nae Mgombea Ubunge wa Jimbo la Makunduchi Wanu Hafidhi Ameir alisema Zanzibar imepata mafanikio makubwa katika Mapinduzi katika maisha ya watu na ustawi wa Jamii pamoja na Maendeleo katika sekta mbali mbali za elimu ikiwemo ujenzi wa skuli za ghorofa, uchumi wa buluu umetoa ajira nyingi Kwa vijana.
Alisema Dk. Samia na Dk. Mwinyi wamefanya kazi kubwa katika miaka mitano iliyopita ikiwemo kudumisha Umoja, mshikamano a utulivu na amani nchini, hivyo wasiwe na wasiwasi Mkoa wa Kusini Kuna kura za kutosha ikiwemo Jimbo la Makunduchi.









0 Comments