Habari za Punde

Katibu Mkuu Fatma Akagua Mradi wa Ujenzi wa Viwanja vya Mchezo wa Mpira

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab akikagua mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo katika uwanja wa Kitogan Wilaya ya Kusini, Unguja akiambatana na baadhi ya  watendaji wa Wizara hiyo.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zanzibar, Fatma Hamad Rajab, amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa juhudi zake kubwa katika kuimarisha na kujenga miundombinu ya michezo nchini.

Amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi zilizomo katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

akitoa pongezi hizo mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku moja ya kukagua miradi mbalimbali ya michezo pamoja na miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa katika mikoa ya Unguja. 

Aidha amesema kazi ya kutengeneza viwanja 17 vya michezo katika wilaya na mikoa yote ya Zanzibar ni ya kujitolea na kuonyesha dhamira ya kweli ya Rais Dk. Mwinyi katika kukuza michezo kwa moyo wa uzalendo.

Aidha, alibainisha kuwa viwanja vya Pangatupu Unguja na Kishindeni Pemba vitakuwa na kiwango Bora vikiwa na hosteli pamoja na vyuo vya wanamichezo kwa ajili ya mafunzo maalum.

Amefahamisha kuwa viwanja hivyo vinatarajiwa kuzinduliwa rasmi katika sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zitakazofanyika tarehe 12 Januari 2026, ambapo vingi miongoni mwao vimefikia hatua ya juu ya ukamilishaji. 

Nae  Afisa Michezo wa Wilaya ya Kusini Unguja, Saum Ali Haji, alisema kukamilika kwa viwanja hivyo kutakuwa chachu ya kuibua vipaji vipya miongoni mwa vijana wa Zanzibar, hasa kutoka Mkoa wa Kusini. 

Alisema vijana watapata nafasi ya kuonyesha uwezo wao na hatimaye kushiriki katika mashindano makubwa ndani na nje ya Zanzibar kutokana na ubora wa miundombinu hiyo.

Aidha, Saum alisisitiza kuwa ujio wa viwanja vyenye michezo mipya kama netiboli na mpira wa kikapu ni fursa kwa skuli na taasisi kuanza kuwafundisha watoto michezo hiyo kwa kuwa ni michezo maarufu duniani. 

Kwa Upande wa Sheha wa Kiongoni Makunduchi, Hadija Kheir Hassan, amesema wananchi wa shehia hiyo wamefarijika  kwa kupelekewa miundombinu hiyo ya michezo, ambayo imeleta matumaini mapya kwa vijana. 

Amesema wanatarajia kupokea wageni na timu mbalimbali za michezo kutoka ndani na nje ya Zanzibar kutokana na ubora wa viwanja hivyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab akikagua mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo katika uwanja wa Mwehe  Makunduchi Wilaya ya Kusini, Unguja akiambatana na baadhi ya  watendaji wa Wizara hiyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab akikagua mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo katika uwanja wa Kitogan Wilaya ya Kusini, Unguja akiambatana na baadhi ya  watendaji wa Wizara hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab akikagua mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo katika uwanja wa Unguja Ukuu, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja akiambatana na baadhi ya  watendaji wa Wizara hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab akikagua mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo katika uwanja wa Pangatupu Wilaya ya Kaskazini ‘B’, Unguja akiambatana na baadhi ya  watendaji wa Wizara hiyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab akikagua mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo katika uwanja wa Pangatupu Wilaya ya Kaskazini ‘B’, Unguja akiambatana na baadhi ya  watendaji wa Wizara hiyo.

Baadhi ya mafundi wakiwa kaitka harakati za ujenzi wa mradi wa viwanja vya michezo katika uwanja wa Mombasa Wilaya ya Magharibi ‘B’ .

 Imetolewa na Kitengo Cha Habari  WHVUM.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.