Habari za Punde

Kitafutwe Kiini cha Udhalilishaji - Naibu Katibu Mkuu Mzee

Na.Omar Hassan - Polisi Zanzibar

Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Katiba na Sheria Afisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mzee Ali Haji  ameshauri kuangaliwa kwa kina sababu zinazopelekea kuongezea kwa vitendo vya udalilishaji wa kijinsia ili hatua za kupunguza udhalilishaji zichukuliwe.

Akifungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa Madawati ya Jinsia na watoto ya Jeshi la Polisi wa Mikoa ya Unguja leo Novemba 10, 2025 huko Chuo cha Polisi Zanzibar amesema Serikali inafanya Jukudi kubwa katika kuzuwia, kubaini na kukabiliana na makosa hayo lakini bado yamekua yakiongezeka.

Nae Afisa Hifadhi ya Mtoto kutoka Shirika la UNICEF Ahmed Rashid Ali amesifu utendaji wa Madawati ya Jinsia na Watoto ya Jeshi la Polisi na kueleza kuwa uanzishwaji wa Ofisi za Dawati katika kila kituo cha Polisi ni miongoni mwa mafanikio katika kushughulikia kesi za udhalilishaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa mtoto Zanzibar, Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Ali Mohamed Othman amesema kumekuwa na mwitiko mdogo wa wananchi kuhudhuria katika vikao vya kufikisha elimu ya kupinga udhalilishaji kwa jamii pindi Watendaji wa Madawati wanapokwenda kutoa elimu kwa jamii.

Kitengo cha Habari,

Makao Makuu ya Polisi,

Kamisheini ya Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.