Ndege ya RwandAir ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar na kupokelewa kwa kuwangiwa maji ikiwa ni ishara ya mapolezi ya ndege hiyo, wakati wa uzinduzi rasmin wa safari mpya inayounganisha Kigali na Zanzibar, uzinduzi huo uliyofanyika 1-disemba 2025.
Itafanyasafari zake mara nne kwa wiki kutoka Kagali na Zanzibar Siku za Jumatatu,Jumatano,Ijumaa na Jumapili
Safari hii mpya inaunga mkono dhamira ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) ya kuimarisha nafasi ya Zanzibar kama kitovu cha usafiri wa anga na utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki. Mkurugenzi Mkuu wa ZAA, Bw. Seif Abdallah Juma, amesema kuwa idadi ya abiria imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni na visiwa vinajiandaa kupokea wageni wengi zaidi na kuendelea kukuza sekta ya utalii.
Wasanii wakitowa burudani wakati wa mapokezi na uzinduzi wa safari ya ndege ya RwandAir uliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Afisa Muendeshaji Mkuu wa RwandAir Ernest Mushi akikata utepa kuashiria kuzindua Safari Mpya ya RwandAir kati ya Kigali na Zanzibar, uzinduzi huo uliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar 1,Disemba, 2025 na (kushoto kwake) Mkurugenzi Mkuu ZAA Seif Abdallah Juma na (kulia kwake) Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe. Patric Mavumba.
Abiria wa Kwanza wa Rwand Air wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, wakitokea Nchini Rwanda wakati wa uzinduzi wa safari hiyo uliyofanyika jana 1,Duswmba 2025.
Afisa Muendeshaji Mkuu wa RwandAir Ernest Mushi akizungumza na kutowa maelezo ya shirika lake wakati Uzinduzi wa Safari za RwandAir kati ya Zanzibar na Kigali uzinduzi huo uliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, 1,Disemba 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa ZAA, Bw. Seif Abdallah Juma akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Safari Mpya ya Ndege ya RwandAir kati ya Kigali na Zanzibar, uzinduzi huo uliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani arume Zanzibar.












Post a Comment