Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Lumumba wamepatiwa mafunzo maalum ya kitaalamu kwa lengo la kuwaongezea ujuzi na kuimarisha huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo, hususan shinikizo la damu na mshtuko wa moyo, katika jitihada za kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wa Zanzibar.
Mafunzo hayo yameandaliwa kwa ushirikiano kati ya Hospitali ya Lumumba, Taasisi ya NSK inayoshirikiana katika uendeshaji wa hospitali hiyo, pamoja na Jumuiya ya Wataalamu wa Moyo kutoka Misri (Egyptian African Heart Association) yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wahudumu wa afya ili waweze kutoa huduma za kisasa na zenye viwango vya kimataifa katika matibabu ya moyo.
Akizungumza mara baada ya kutolewa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Marijani Msafiri, amesema hatua ya kuwapatia mafunzo madaktari na wauguzi katika kuonesha dhamira ya dhati ya kuimarisha huduma za kibingwa nchini na kueeleza kuwa kuwekeza katika mafunzo ya wataalamu wa afya ni hatua muhimu katika kuimarisha sekta ya afya na kufanikisha kupunguza kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.
Dkt Marijani amesema Wizara ya Afya kupitia Hospitali ya Rufaa Mkoa Lumuba kupitia Taasisi ya NSK wataendeleza ushirikiano na Egyptian African Heart Association huku mipango ya mafunzo ikiendelea zaidi ili kuhakikisha huduma za matibabu ya moyo yanazidi kuimarika na kuwafikia wananchi wengi na kwa wakati.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa ajali na dharura Moiz Adamji kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Lumuba amewata wananchi wa Zanzibar kuwa na tabia ya kupima maradhi ya Presha na kisukari mara kwa mara ili kujibaini mapema na kupata matibau mapema kwa usahihi ambapo alisema wagonjwa karibu ya asilimia 70 wanaofika Lumumba wanamaradhi hayo.
Nae Dkt Zainab Bwanakheir Hassan ambae ni mtaalamu magonjwa ya dharura na wagonjwa mahatuti katika Hospitali ya Lumuba amesema mafunzo waliyapata yatasaidia kwenda kuanzishwa kwa huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo katika Hospitali hiyo na kupunguza wagonjwa kupelekwa katika matibabu nje ya nchini.



0 Comments