6/recent/ticker-posts

UANZISHWAJI WA VIWANGO VYA MWANI KIMATAIFA

Na Miza Kona Maelezo Zanzibar 11/03/2026

Mkurugenzi wa Uandaaji wa Viwango, Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Hafsa Ali Slim amewataka wadau mwani kuipitia na kuijadili rasimu ya kiwango cha mwani ili kutoa maoni sahihi yatakayoewesha kupata viwango cha kizuri cha kimataifa chenye kunufaisha wakulima na wafanyabiashara wa zao hilo nchini.

Akifungua mkutano na wadau mwani katika kupitia na kutoa maoni ya viwango vya mwani katika ukumbi wa Taasisi hiyo Maruhubi amesema lengo la mkutano huo kupata ni maoni ambayo yataondosha vikazo kwa wazalishaji na wafanyabiashara.

Amesema katika rasimu iliyopita vilikosekana vitu muhimu katika kupanga viwango vyenye kukubalika kimataifa hivyo baada kupata maoni na umuhimu wake wadau wamejadili na kuingiza viwango vya mwani  kwa kuweka madaraja ya mwani ili kupata ubora na kuleta mafanikio kwa wadau wa mwani.

“Leo tumefanya mapitio ya kiwango cha mwani kwani kiwango tulichofanya mwanzo tumepokea maoni ambayo ni muhimu sana ambayo hatukuweza kusema tunaiacha masuala ya gredi kama tunavyojua masuala ya mwani yapo kwenye ambapo kuna  juu zaidi, kati na upo chini hapo mwanzo lilikuwa halipo kwenye viwango sasa hivi tumelijumuisha kwenye viwango na tumetaka wadau ambao ni wazalishaji na wasafirishaji watupe maoni yao ili baadae isijekuwa na kikwazo chochomkatika kufanya biashara ya mwani”, ameeleza Mkurugnzi nhyo.

Akitoa mada ya Kupitia na kutoa maoni ya viwango Mwezeshaji kutoka Wakala wa Viwango Zanzibar Arabia Makame Haji amesema kwa sasa ZBS imefanya mapitio ya rasimu ya kiwango mwani ili kuongeza kipengele cha madaraja katika rasimu hiyo ambapo kiwango chamwa kinaelezea vigezo maalum, mbinu za kuchukulia sapli na vipimo vya mwani mkavu. .

Mwezeshaji huyo ameelezea vigezo vya viwango mwani mkavu ni kuwa mwani  uwe wa aina moja, uwe umekomaa kwa zaidi ya mabanvua matatu (siku 45), usiwe na maradhi na uwe na rangi ya aina ya mwani husika.

“Vifungashio vya mwani mkavu vinatakiwa view vyenye ubora wa kuhifadhi bidhaa na lugha ya kifungashio inatakiwa iwe kwa Kiswahili au kiengereza, lugha ya ziada inaruhusiwa kulingana na soko husika”, amefahamisha Mweaeshaji Arabia.

 Nao washiriki wa mkutano wamesema kuwa ni muhimu kuwa viwango vinavyohitajika kuanzia  kwa mzalishaji hadi kwa wasafirishaji pia viwango vya mwani vitakuwa vizuri iwapo vitakwenda sambamba na bei ya mwani

Aidha wameeleza kuwa kuwekwa viwango katika zao la mwani kutasaidia na kuweza kumlinda mkulima wa zao la mwani pamoj na mfanyabiashara na kuepuka usumbufu wa kupoteza thamani ya zao hilo.   

Post a Comment

0 Comments