Habari za Punde

DK.Shein Afungua Kongamano la Utafiti na Ubunifu Zanzibar Beach Resort

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akitoa hutuba yake wakati alipolifungua Kongamano la Utafiti na Ubunifu leo, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,(wa kwanza kulia) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa,( SUZA), Prof, Idrisa A.Rai, (kushoto) ni Dk.Hassan Mshinda,Mkurugenzi  Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia  Tanzania,akifuatiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed,alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,kulifungua Kongamano la Utafiti na Ubunifu,katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort leo
 Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Prof, Idrisa A.Rai,alipokuwa akitoa salamu zake wakati wa Kongamano la Utafiti na Ubunifu,lililofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach
Resort na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein
 Baadhi ya wadau mbali mbali walioshiriki katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) akitoa hutuba yake wakati alipolifungua leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akiangalia mashine ya ubunifu wa Umeme wa kufua kutumia (Upepo hewa) ambayo imebuniwa na Ali Mahmoud Ali,(kushoto)  wakati maonesho katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu,lililofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipata maelezo yanayohusu Mfumo wa kuhifadhi taarifa za Hospitali,(HOSPITAL MANAGEMENT SYSTEM) kutoka kwa Editha Dismas Lyimo, wakati   alipotembelea  maonesho katika Kongamano la Utafiti na bunifu,lililofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipata maelezo kutoka kwa David Mung’ong’o, wa Blackmark-Poultry Expo Tanzania, Kituo kinachoshuhulikia Kuku (Ndege wanaofungwa),Ushauri,Maonesho ya wadau kama wafugaji,watengenezaji vyakula vya mifugo,watoa huduma,wanaouza Dawa,vifaa,watotoleshaji vifaranga,wakati   alipotembelea  maonesho katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu,lililofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipata maelezo kutoka kwa Alex Maharindo, wa Kampuni ya  BR-Solution,ambayo inashuhulika na utoaji wa Taarifa kwa watumiaji wa simu za mikononi, wakati   alipotembelea maonesho katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu,lililofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Dk.Hassan Mshinda,Mkurugenzi  Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania,wakati alipotembelea maonesho katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu,lililofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,(Picha naRamadhani Othman Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.