Sehemu ya wizi wa maji kutoka katika mtandao wa DAWASCO unavyoonekana kufanywa katika kiwanda cha kutengenezea Betri cha Bahari Chemicals Ltd.
  
Ikiwa
siku chache tu zimepita baada ya shirika la Majisafi  
 
na Majitaka Dar es salaam
(Dawasco) kubaini wizi mkubwa wa Maji kutumika katika shamba la mboga mboga na
matunda katika chuo cha Islamic kilichopo Boko ununio jijini Dar es salaam.
Dawasco imebaini wizi mwingine wa Maji katika kiwanda cha kutengeneza Maji ya
betri cha Bahari Chemicals Ltd kilichopo kurasini wilaya ya Temeke jijini Dar
es salaam. 
  
Akizungumzia
tukio hilo meneja wa Dawasco Temeke, Bw.  
 
Deogratius Rwegasira, amethibitisha
kutokea kwa wizi huo  
 
ambapo kiwanda hicho kilikuwa kimejiunganishia Maji bila  
 
kibali cha Dawasco na kwamba hawakuwa na mita wala  
 
akaunti namba inayoonyesha
kiasi cha Maji kinachopita  
 
katika system ya Maji iliyopo, na baada ya kufanya  
 
mawasiliano na Mkurugenzi wa kiwanda hicho  
 
Bw.Devendra Singh Parmar amekiri
kutumia Maji hayo  
 
kinyume na taratibu . 
“Baada
ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa kiwanda hiki  
 
kimekuwa kikituibia Maji yetu
kwa muda mrefu, mmiliki wa  
 
kiwanda amekubali kosa,lakini akisema kwamba wenyewe  
 
ni wageni hapa hawana zaidi ya mwaka mmoja tangu  
 
waanze kazi.hivyo hawakujua
taratibu za kufuata”. Alisema  
 
Bw. Rwegasira. 
  
Aidha
meneja wa kiwanda hicho, Bw. Abdul Gulam, amekiri  
 
kuihujumu Dawasco kwa kuiibia
Maji, lakini amesema kuwa  
 
wao ni wapangaji tu wamepanga katika eneo hilo na
wana  
 
muda wa miezi saba tangu wahamie kiwandani hapo,  
 
walikuta wizi huo wa Maji
ukifanyika katika kiwanda hicho  
 
na
hawakujua taratibu husika za kufuata ili wapate huduma  
 
ya Maji kihalali. 
  
“Sisi
tumekubali kuwa tulikuwa tunatumia Maji ya  
 
DAWASCO bila kuyalipia, lakini sio
sisi ambao  
 
tuliounganisha bomba hili, wapangaji waliopita  
 
walijiunganishia Maji
haya hivyo tunaomba tulimalize hili, ili  
 
tuanze kuwa wateja wenu rasmi” alisema
Bw.Gulam. 
  
Aidha
bwn Gulam ameainisha kuwa wao kama wamiliki wa  
 
kiwanda wamekubali kulipa faini
iliyotolewa na DAWASCO  
 
ya Shiling million 3.5 ili warudishiwe huduma kama
wateja  
 
wengine na waweze kuendelea na biashara. 
  
Vitendo
vya uhujumu wa Miundombinu ya Maji hususani  
 
wizi wa Maji unaendelea kuwa
changamoto kwa  
 
DAWASCO licha ya kampeni na elimu inayotolewa kila siku  
 
juu ya
uhalali na utaratibu wa kuungiwa huduma ya Maji  
 
inayotolewa na DAWASCO. 
  
Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii. 
 | 
No comments:
Post a Comment