Habari za Punde

Mwili wa Mbunge Leticia Nyerere Wawasili Jijini Dar es Salaam kwa Mazishi yake Kufanyika Butiama Mkoani Mara Kesho Kutwa.

 Askari wa Bunge wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere aliyefariki nchini Marekani alikokuwa akitibiwa mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Mwili huo kesho utaagwa nyumbani kwa Mwalimu Nyerere Msasani  kabla ya kusafirishwa kwenda Butihama mkoani Mara kwa mazishi yatakayofanyika keshokutwa.
 Mwili huo ukiingizwa kwenye gari maalumu katika uwanja huo.
 Ndugu jamaa na marafiki wakijadiliana jambo wakati wa kuupokea mwili huo.
 Ndugu, jamaa, marafiki na watoto wa marehemu wakisubiri kuupokea mwili wa mpendwa wao.
 Mume wa marehemu, Madaraka Nyerere akizungumza na wanahabari baada ya kuupokea mwili huo uwanjani hapo.
Mtoto wa marehemu (kulia), akifarijiwa na mmoja wa ndugu wakati wakienda kupanda gari kabla ya kuondoka uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.