Habari za Punde

ZU YAONGOZA KUCHEZA FAINALI MARA NYINGI ZAHILFE CUP, KESHO KISASI CHENGINE KWA AFYA, ANGALIA HISTORIA YA TIMU ZILIZOTINGA FAINALI MIAKA YOTE

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Fainali ya Mashindano ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar (ZAHILFE CUP) inatarajiwa kusukumwa kesho majira ya saa 10:00 za jioni kwenye uwanja wa Amaan kati ya Mabingwa wa watetezi wa Mashindano hayo Chuo cha Zanzibar Univeristy (ZU) dhidi ya Chuo cha Afya Mbweni.

Historia ya Mashindano hayo ambayo kwasasa ni Mashindano ya 5 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013, ZU ndio timu iliyocheza mara nyingi fainali baada ya kucheza mara 3 na kufungwa mara mbili wakishinda mara 1 ambapo kesho itakuwa fainali yao ya 4 kucheza katika Mashindano hayo.

Bado rikodi zinaonesha kuwa ZU ni Chuo Bora baada ya kufika fainali miaka yote isipokuwa mwaka mmoja (2014) kwenye miaka 5 ya Mashindano hayo.

Afya Mbweni hii ni mara ya pili kufika fainali kufuatia mwaka 2013 kuwafunga ZU bao 1-0 ambapo kesho ZU anataka kulipa kisasi huku Afya wanataka kuendeleza kuwafunga tena fainali ZU.

HISTORIA YA ZAHILFE
2013  AFYA MBWENI 1-0 ZU
2014 CHWAKA PENALTI 5-4 ZITOD, DAKIKA 90 WALITOKA 1-1
2015 SUMAIT PENALTI 5-4 ZU, DAKIKA 90 WALITOKA 0-0
2016 ZU 4-2 CHWAKA
2017 ZU v/s AFYA?.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.