Habari za Punde

Wagombea Uwakilishi wa CCM Ndg Ramadhn Hamza Chande na wa Chama Cha ADA TADEA Sabry Ramadhan China Wakutana Katika Kituo cha Skuli ya Jang'ombe.

Wagombea Uwakilishi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang'ombe Zanzibar wakutana katika Kituo cha Kupigia kura Skuli ya Jang'ombe kulia Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Ramadhan Hamza Chande na kushoto Mgombea wa Chama Cha ADA TADEA Ndg. Sabry Ramadhan China, wakisalimiana na kupongezana wakati zoezi la upigaji kura likiendelea katika Vituo mbalimbali vya jimbo hilo. wakiwa katika viwanja vya Skuli ya Jang'ombe Sekondari wakitembelea kujionea zoezi hilo la kupiga kura likiendelea kwa Amani na Utulivu kwa Wananchi waliojitokeza kupiga kura yao.  
Mgombea wa CCM Ndg Ramadhan Hamza Chande na wa Chama Cha ADA TADEA Ndig Sabty Ramadhan China wakisalimiana walipokutana katika Kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Sekondari ya Jang'ombe Zanzibar. 
Mgombea Uwakilishi katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Jang'ombe Zanzibar Ndg. Sabry Ramadhan China akitembelea kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Sekondari ya Jang'ombe Zanzibar, wakati zoezi hilo likiendelea katika vituo vya jimbo hilo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.