Mwenyekiti wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt Abdulla Makame akisisitiza jambo wakati walipotembelea
mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Horohoro ikiwemo upande wa pili wa
nchi ya Kenya
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akifuatilia jambo wakati wa ziara hiyo
Sehemu ya watumishi wa TRA mkoa wa Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali
Mwenyekiti
 wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
 Abdulla Makame kushoto akisalimiana na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga
Specioza Owure wakati walipoingia kwenye Kituo cha Forodha Horohoro.
WABUNGE
 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdulla Makame na Mhandisi Mohamed
Habibu Mnyaa  katikati wakiangalia bidhaa mbalimbali mpakani hapo.
Mbunge
 wa Bunge la Afrika Mashariki Mhandisi Mohamed Habibu Mnyaa katikati
akinawa na santize kabla ya kuingia kwenye ofisi mbalimbali zilizopo
mpakani hapo.
Meneja
 wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kulia akiwa na Mbunge  wa Bunge la
Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdulla Makame wakitoka nje mara baada ya
kufanya ziara yao.
 Wakipata picha ya pamoja mara baada ya kutembelea eneo hilo
 Wakiwa kwenye picha ya pamoja na Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
WABUNGE
 wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wametembelea mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Horohoro –Lungalunga
kuangalia umeathirika vipi kutokana na janga la Virusi vya Corona na
hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa kuweza kukabiliana nao huku
wakiridhishwa na hatua zinazochukuliwa. 
Mpaka wa Horohoro upo
wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga na Kenya ambao umekuwa ukitumiwa na
wananchi wa nchi hizo mbili kuweza kuvuka upande mmoja hadi mwengine
lakini hivi sasa inaelezwa huwezi kuvuka bila kuwekwa chini ya uangalizi
 kwa kipindi cha siku 14. 
Akizungumza mara baada ya kutembelea
eneo hilo  hivi karibuni Mwenyekiti wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Abdulla Makame ambayo pia walikuwa
wameambatana na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure huku
akizipongeza mamlaka zilizopo mpakani hapo kutokana na hatua inazochukua
 kukabiliana na janga hilo lakini kwa kuzingatia taratibu zilizotolewa
na Serikali. 
Mwenyekiti huyo pia aliwapongeza watumishi
wanaofanya kazi kwenye sekta ya afya nchini kutokana na kuwa mstari wa
mbele kutoa huduma ikiwemo kuweka maisha yao rehani kuhakikihs
wanatuokoa na janga hilo hatari ambalo limekuwa tishio kubwa duniani. 
Aidha
 alisema mpaka sasa nchi haijafunga mipaka yake na watu wanaendeela
kuvuka lakini kwa tahadhari ya afya wanaovuka wataendelea kuwekwa chini
ya uangalizi kwa siku 14 ili waweze kujiridhika kama ana maambukizi au
la . 
“Mpaka sasa hapa kwetu nchi haijafunga mipaka yake sababu
serikali inataka bidhaa muhimu ikiwemo vifaa tiba kwa kipindi hiki
vinahitajika vitaendelea kuvuka lakini watu wanaovuka watakwenda
karatini”Alisema Dkt Abdulla. 
Mwenyekiti huyo alisema kwamba sio
 kwamba watu wanazuiwa ili waonewe wanachoifanya ni kupambana na janga
la kitaifa ambalo limefanya mataifa makubwa watu wanalia, wanakufa hali
ni hatari na lazima hatua hizo zichukuliwe. 
“Lakini pia
tumeambiwa hapa kwamba abiria wakivuka wanakaa karantine siku 14 katika
uangalizi kabla ya kuvuka tumeonyeshwaa maeneo na mengine tumeambiwea
yapo Tanga mjini kabla ya kuendelea na safari zao hilo zoezi lilikuwa ni
 kuangalia abiria”Alisema 
“Madereva walikuwa na utaratibu
tofauti kwa sababu wanapeleka mizigo na walisema hawataki mizigo isivuke
 kutokana na baadhi yake ni vifaa ikiwemo tiba na vyakula ambavyo
vinahitajika kila siku na kuweka maisha yakawe sawasawa “Alisema 
Mwenyekiti
 huyo alisema kwamba lakini waraka namba 2 umetoka na kwa sasa madereva
nao watakuwa wakikaa karantine huo waraka utaanza kutekeleza kutokana na
 hilo wameona maelekezo yanazidi kuwa makali lakini pamoja na ukali
wanasema mipaka bado ipo wazi na bidhaa muhimu zitaendelea kuvuka. 
Hata
 hivyo alisema watatumia utaratibu mwengine kwamba ama gari zishushe
mizigo mipakani ipandishwe magari mengine au gari ije ibadilishe
madereva mipakani na kuwekwa dawa na madereva kubaki kwenye nchi zao. 
“Kimsingi maelekezo ya serikali yanaendelea kufuatwa na mpaka sasa
kwenye mpaka huo hajapatikana mgonjwa yoyote wa Corona lakini tumeambiwa
 wapo karatine watu 47 na watu wanne walishukiwa kuonyesha dalili
walipimwa wakawa hawana na waliruhusiwa”Alisema 
Awali
akizungumza kwa upande wake Mbunge mwengine wa Bunge hilo Mhandisi
Mohamed Habibu Mnyaa alisema wamefika eneo hilo kwa lengo la kuona
uelewa upo kiasi gani na taratibu zilizotangazwa na serikali za
kujilinda na virusi vya Corona umeeleweka kiasi gani na watu wanayafuata
 kwa kiasi gani. 
Alisema wao kama wabunge wa Bunge la Afrika
Mashariki wamelazimika wote kufanya kazi ndani ya nchi zao kushirikiana
na serikali na wananchi kuhusu kupiga vita maradhi ya virusi vya Corona
kwa hiyoi kwa upande wa Tanzania wamegawana vikundi vya watu wawili
wawili maeneo mengine mmoja kutembelea mipaka mbalimbali iliyopo nchini
lengo kusaidia uelewa wa wananchi kupiga vita maradhi hayo.
 Naye
 kwa upande wake Afisa Afya Mfawidhi Huruma Kimaro alisema katika mpaka
huo hakuna mtu yoyote anayepita na wanaofika hapo wanapelekwa karatini
na mpaka sasa watu 47 wapo karatine huku akieleza kwamba walipata
washukiwa wanne walipopelekwa maabara walikuwa hawajaambukizwa
waliwaruhusu na kuwapa maelekezo ikiwemo kutoa ushauri kwao kwa
kuendelea kuwa mabalozi wazuri.
 
No comments:
Post a Comment