Habari za Punde

SEKTA YA AFYA MAHENGE ULANGA YAPIGWA TAFU NA SHIRIKA LA SOLIDAR MED

Mratibu wa Afya ya Mama, Baba na Mtoto kutoka Hospitali ya Wilaya ya Mahenge Patricia Haule (kushoto) akiwaonesha baadhi ya majengo yaliyofanyiwa ukarabati na Shirika la Solidar Med Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs chini ya Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati walipotembelea mradi wa ukarabati wa Wodi ya Mama na Mtoto Hospitalini hapo katika kuangalia Miradi inayotekelezwa na NGOs mkoani Morogoro.
Mratibu wa Afya ya Mama, Baba na Mtoto kutoka Hospitali ya Mahenge Patricia Haule (kushoto) akifafanua jambo kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs chini ya Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati walipotembelea mradi wa ukarabati wa Wodi ya Mama na Mtoto Hospitalini hapo katika kuangalia Miradi inayotekelezwa na NGOs mkoani Morogoro. 
Mratibu wa Afya Msingi wa Shirika la Solidar Med Mary Yagala (kulia) akifafanua jambo kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs chini ya Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati walipotembelea miradi inatekelezwa na NGOs mkoani Morogoro.
Moja ya jengo liliofanyiwa ukatabati na Shirika la Solidar Med katika Hospitali ya Mahenge mkoani Morogroro.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiiano Serikalini WAMJW

Na Mwandishi Wetu Mahenge
Shirika la Solidar Med limetoa jumla ya Shillingi millioni 250 kujenga na kukarabati majengo ya Mama Baba na Mtoto na kusaidia vifaa tiba katika Hospitali ya Mahenge na Zahanati ya Ilonga zilizopo Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro.
Hayo yamebainika wakati wa zoezi la kutembelea miradi inayotekelezwa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Mkoa wa Morogoro liliofanywa na Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs nchini.
Akielezea miradi ya ujenzi na ukarabati iliyotekelezwa na Shirika la Solidar Med Mratibu wa Afya ya Msingi wa Shirika hilo Mary Yagala amesema kuwa wamelenga kuboresha afya ya Mama na Mtoto wakilenga kupunguza vifo vya wakinamama na watoto katika Wiaya ya Ulanga.
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha wahudumu wa Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati katika Wilaya ya ulanga wanatoa huduma katika mazingiramazuri Shirika hilo linatoa mafunzo ya kuwawezesha kutoa huduma katika ubora unaotakiwa hasa kwa Mama na Mtoto.
“Tunaendelea kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga katika kuhakikisha tunakuwa na miundombinu na vifaa muhimu ili kuokoa maisha hasa ya Mama na Mtoto” alisema
Aidha amesema kuwa Shirika hilo limejenge wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya Mwaya ambapo imewezesha kuchukua wanawake wengi ambapo kwa mwanzo jengo lililokuwepo lilikuwa linachukua watu wachache.
Kwa upande wake Mratibu wa Afya ya Mama,Baba na Mtoto wa Hospitali ya Mahenge Patricia Haule amesema Shirika la Solidar Med limesaidia kuwepo na mazingira mazuri ya wahudumu kutoa huduma kwa wakina Mama na mtoto katika Hospitali ya Mahenge.
“Tumefarijika sana kwa hatua hii ya Shirika la Solidar Med kuona haja ya kujenge na kukarabati majengo ya kutolea huduma ya Mama na Mtoto katika Halmashauri ya Wilaya ya ulanga”alisema
Kwa upande wao Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs ncini wamelipongeza Shirika hilokwa hatua ya kuhakikisha inasaidiana na Serikali katika kupunguza vifo ya akina Mama na Mtoto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.