Habari za Punde

WIZARA YA ARDHI YAPATA TUZO KATIKA KONGAMANO LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

 

Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti na Tuzo ya kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Ageline Mabula kwa wizara yake kushika nafasi ya tatu kwa upande wa kundi la wizara wakati wa kongamano hilo lililofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri (Waliosimama nyuma) wakati wa Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika jijini Dodoma
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara (Walisimama nyuma) wakati wa Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika jijini Dodoma

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepata Cheti na Tuzo katika Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kushika nafasi ya tatu kwa upande wa kundi la Wizara.

Tuzo hiyo imekabidhiwa Sept 19, 2022 wakati wa Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi lililofanyika jijini Dodoma.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano.

Katika kongamano hilo Waziri Mkuu aliwataka wadau wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kuongeza nguvu katika kutoa huduma za uwezeshaji hasa maeneo ya pembezoni ya miji na vijijini ili kufikia malengo ya nchi katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Aidha, aliitaka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuongeza kasi katika kupima na kurasimisha maeneo mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.