Menu

Thursday, July 10, 2025

Wanawake wa Dar es Salaam Waomba Elimu Zaida Kuhusu Haki


WANAWAKE Jijini Dar es salaam wameomba elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora izidi kutolewa kwenye mikusanyiko ya wanawake kwani wao mara nyingi wamekuwa wakikosa fursa ya kupata elimu hiyo hasa katika mikutano inayoandaliwa na viongozi wa Serikali kutokana na majukumu waliyo nayo.

Rai hiyo imetolewa na wanawake waliotembelea banda la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwenye maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.

"Tumejifunza mengi leo kuhusu haki zetu kama wanawake, tunaomba elimu hii itufikie hadi kwenye vikundi vyetu vya kina mama, kwani mara nyingi tunashindwa kuifikia mikutano inayoandaliwa vijijini ama mitaani kutokana na shughuli nyingi za jamii majumbani, lakini elimu ya haki  ikitukuta kwenye vyama vyetu huwa tunalazimika kwenda kwasababu huwa haviwahusu wanaume”. alisema mama mmoja mkaazi wa …aliyetembelea banda ya THBUB, viwanja vya sabasaba.

Kwa upande wao maofisa wa THBUB waliielezea Tume kwamba inaendeleza juhudi na kuhakisha elimu hiyo inawafikia wananchi wa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake, kupitia maonesho hayo, warsha, semina na makongamano ili kufikisha kwa jamii ujumbe wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Mmoja wa maofisa hao, Innocent Amani Afisa Uchunguzi mkuu wa THBUB ameeleza kuwa THBUB  inatambua changamoto zilizopo katika kufikisha elimu hiyo kwa baadhi ya maeneo, lakini inaendelea kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo kuhakikisha kwamba elimu ya haki za binadamu inawafikia Watanzania wote bila ubaguzi.

No comments:

Post a Comment