Miaka Mitano ya Mafanikio zaidi katika Huduma kwa Wananchi Inakuja Ikiongozwa na Dr.Samia Suluhu Hassan.
Maneno hayo yamesemwa na Mgombea pekee wa Nafasi ya Ubunge jimbo la Chalinze alipokuwa kwenye ziara ya Kujitambulisha na kutambulisha wagombea Udiwani wa Chama Cha Mapinduzi katika kata za Halmashauri ya Chalinze.
Akizungumza na Wanachama katika tarafa ya Kwaruhombo inayoundwa na kata za Kibindu, Mbwewe na Kimange, Mgombea Kikwete alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwa ushirikiano uliozaa mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Maboresho na Ujenzi Mkubwa wa Miundombinu, Barabara na usafirishaji, Kilimo, uwezeshaji Wananchi, Ujenzi wa Viwanda, na Upatikanaji wa fursa mbalimbali ambapo alisema kuwa mafanikio haya yote yanatokana na Ushirikiano mzuri na mkubwa waliompa yeye, Madiwani na Mh. Rais katika kufikia tamaa za Wananchi wa Jimbo na halmashauri hiyo.
Pamoja na mafanikio makubwa Mgombea Kikwete aliwashukuru wananchi kwa kumpa nafasi na kumuheshimisha kwa mfanya awe peke yake; japo kwake alisema kuwa kitendo hiki sio tu kinaonyesha imani kubwa kwa uongozi wake ila ni salamu za wanachalinze kuridhishwa na utendaji kwa upande mmoja na kuonyesha imani kuwa changamoto zilizobaki watazimalizia. Akizungumza pia aliwaomba wananchi kwa imani hiyo wampe madiwani ambao watakwenda kushirikiana kufanya kazi kujibu matumaini hayo ya wananchi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa Kata hizo wamempongeza na kumshukuru sana Mbunge wao huyo anayemaliza muda wake kwa ushirikiano na jitihada za dhati alizozifanya kuwahakikishia maendeleo yanapatikana lkn kudumisha ushirikiano na wananchi.
Mgombea Ndugu Kikwete anaendelea na ziara jimboni hapo.
No comments:
Post a Comment